Friday, May 2, 2014



MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Mbrazil, Neymar, amesema anafurahia mahusiano yake mazuri na mchezaji mwenzeka wa klabu hiyo, Lionel Messi.
Bosi wa Barca, Gerardo Martino Tata ameshindwa kuwatumia wawili hao kama ilivyotarajiwa kutokana na kukumbwa na majeruhi ya mara kwa mara msimu huu.
Kumekuwepo na taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa wawili hao hawana mahusiano mazuri na hawataki hata kuonana ana kwa ana, lakini Neymar amesisitiza kuwa yeye na Messi ni marafiki wakubwa ndani na nje ya uwanja.
“Hatuchezi wote kila mchezo, lakini nadhani tumejenga uhusiano mzuri tena wakustaajabisha”. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amesema wakati wa mahojiano na CNN.
“Watu wengine walisema tusingeelewana, lakini ulikuwa uongo. Ni mtu rafiki sana, ni nyota ninayempenda”.
Neymar alicheza katika fainali ya Copa del Rey aprili 16 mwaka huu ambapo Barcelona walicharazwa mabao 2-1 na Real Madrid , lakini alipata majeruhi na ilithibitishwa kuwa atacheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini kwake Brazil.
Neymar aliongeza: “Nitakuwa fiti kwa fainali za kombe la dunia. Tatizo pekee ni kwamba siwezi kuisaidia Barcelona. Natarajia kubeba kombe la dunia na nitawasaidia wenzangu kutimiza malengo haya”.
“Najua wajibu wangu kwa timu yangu ya taifa, kama ilivyo kwa wenzangu. Tumekuwa wamoja na tutasaidiana sana, tunajiandaa kutwaa taji la kombe la dunia”.
Mbrazil huyo pia ametumia nafasi hiyo kueleza masikitiko yake juu ya utata wa uhamisho wake uliofanyika  mwezi juni mwaka jana kutoka klabu yake ya zamani ya Santos kujiunga na Barca.
“Kila kitu kilikuwa sahihi na hatukufanya makosa hata kidogo”. Neymar aliendelea.
“Jinsi ambavyo Santos walilichukulia suala langu waliniacha katika huzuni, lakini nitafanya nini”
“Siwezi kuwajibia, lakini nazungumza kivyangu na kwa ajili ya baba yangu kwamba hatua walizotaka kuchukua kutatua tatizo hili hazikupendeza”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video