
Kazini: Mfungaji wa bao la kwanza la Liverpool, Joe Allen (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Palace, Marouane Chamakh

Ajabu: Gayle akishangilia na Yannick Bolasie, baada ya kuchafua hali ya hewa kwa Liverpool uwanja wa Selhurst Park

Manyoya tu: Kipa wa Palace, Julian Speroni akishindwa kuokoa mpira uliopigwa na Daniel Sturridge na kuifungia Liverpool bao la pili.

Suarez akishangilia kufikia rekodi ya Alan Shearer na Cristiano Ronaldo ya mabao 31 kwa msimu mmoja

NDOTO za majogoo wa jiji, klabu ya Liverpool kufuta ukame wa miaka 24 bila kikombe zimeanza
kufifia baada ya usiku huu kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya wenyeji Crystal
Palace katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England.
Kwa matokeo ya mchezo huo, Liverpool wanapanda
kileleni baada ya kufikisha pointi 81, huku Manchester City wenye michezo
miwili mkononi wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 80.
Majogoo wa jiji walikuwa wa kwanza kuandika bao la
kuongoza dakika ya 18 kipindi cha kwanza kupitia kwa Joe Allen, baadaye dakika
ya 53, Daniel Sturridge akifunga bao la pili, huku bao la tatu likifungwa
dakika ya 55 kupitia kwa Luis Suarez.
Wakati Liverpool wakiamini watashinda mechi ya
leo, kibao kilibadilika dakika ya 79 baada ya Damien
Delaney kusawazisha bao la kwanza.
Ikiwa kama utani vile, dakika ya 81 Dwight Gayle
aliisawazishia Palace bao la pili.
Liverpool wakazidi kuchanganyikiwa na kuona dakika
haziendi. Mnamo dakika ya 88 Dwight Gayle
aliandika bao la tatu na mechi kuisha kwa sare ya 3-3.
Baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, Luis
Suarez aliangua kilio kikubwa kwa kuamini kuwa kuna asilimia kubwa wameshaweka
reheni mbio zao za ubingwa.
Liverpool wamebakiwa na mechi moja mkononi ambayo
wakishinda watafikisha pointi 84, wakati Man city wakishinda mechi zao mbili watafikisha
pointi 86 na kutwaa taji.
Kama Man City watashinda mechi moja na kufungwa
moja, halafu Liverpool wakashinda mechi ya mwisho, basi majogoo hao wa jiji
watafanikiwa kutwaa ubingwa.
Liverpool wanategemea muujiza wa soka kutokea.
0 comments:
Post a Comment