Saturday, May 3, 2014



 Staz
Na Baraka Mpenja, Dar e salaam
CHAMA cha soka Mkoani Mbeya, MREFA kimewaomba mashabiki wa soka mkoani humo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars  katika mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi hapo kesho uwanja wa Sokoine.
Katibu mkuu wa MREFA, Seleman Haroub ameueleza mtandao huu kuwa Mbeya wamepata bahati ya kuiona Taifa stars kwa mara ya kwanza ikicheza katika ardhi yake, hivyo wasiwaangushe Watanzania wenzao.
“TFF wametuamini na kutuletea pambano hili la kimataifa. Ni fursa nyingine kwa mashabiki kuwaonesha watanzania kuwa Mbeya wanapenda Mpira”.
“Wajitokeze kesho kwa wingi kuishangilia Taifa stars. Kuna mikoa mingi ambapo mechi hii ingechezwa, lakini jitihada za MREFA kwa kushirikiana na wamiliki wa uwanja wa Sokoine zimeleta mechi hii”.
“Hii ni mechi ya Kimataifa, ujue TFF wameridhishwa sana na mazingira ya uwanja wa Sokoine kwa sasa, na ndio maana wameamua kuileta Taifa stars”
“Sasa wana Mbeya tusiwe nyuma ili siku zijazo tuendelee kupata nafasi kama hii iliyozoeleka kwa mikoa ya Arusha (miaka ya nyuma), Mwanza na siku zote Dar es salaam”. Alisema Haroub.
 AZAMFC1
Kwa upande wake meneja wa uwanja wa Sokoine, Modestus Mbande Mwaluka alisema maandalizi ya uwanja yamekamilika kwa asilimia 95.
“Jana tumefanya kazi kubwa ya kumalizia kupata rangi vyumba vya kisasa vya kubadilishia nguo.”
“TFF waliagiza hilo lifanyike kabla ya mechi. Tumeshirikiana na wadau na kukamilisha zoezi hilo”
“Unajua Mbeya,  watu wanapenda mpira na kama umewahi kufika kwenye mechi za Mbeya City basi utaamini hilo”.
“TFF wametuamini na wametuletea timu ya Taifa, nasisi tumejipanga kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri”.
“Uwanja uko tayari na nikiwa meneja malengo yangu ni kuhakikisha tunapata mechi nyingi za kimataifa”. Alisema Mwaluka.
Kiingilio katika mechi hiyo ya kwanza kwa kocha mpya wa Taifa stars, Mart Nooij  kitakuwa sh. 5,000 wakati tiketi zitauzwa siku ya mchezo kuanzia saa 2 asubuhi katika vituo vya Uyole, Mwanjelwa,, Mbalizi, Stendi Kuu, Holiday Inn na Uwanja wa Sokoine.

Magari yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni ya wachezaji, gari la wagonjwa, gari la zimamoto na gari la waamuzi pekee.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video