KOCHA
wa Chelsea, Mreno, Jose Mourinho amelaumu kuwa majeruhi katika kikosi chake na
uchovu kwa wachezaji imekuwa sababu ya kupoteze mechi dhidi ya Atletico Madrid.
The
Blues walitandikwa mabao 3-1 Stamford Bridge usiku wa jana na kutolewa katika
hatua ya nusu fainali ya UEFA kwa
wastani wa mabao 3-1 kufuatia suluhu ya bila kufungwa Vicente Calderon.
Mourinho
amewasifu wachezaji wake kwa kupigana kwasababu kwa muda wote walikuwa
wanajitahidi kujiweka fiti kwa ajili ya mechi, lakini kulikuwa na matatizo
mengi kwa Chelsea.
“Nilisema
jumanne, wachezaji wangu walikuwa tayari na walitaka kuwa tayari kwasababu
walitaka kucheza”.
“Walitaka
kusaidia, kwasababu walijua kuwa tuko karibu na fainali, lakini wakati huo huo
tulikuwa na matatizo mengi”. Mourinho aliwaambia waandishi wa habari .
“Kwa
hiyo kila mchezaji alijituma kadri awezavyo na Eto`o hakuwepo muda mwingi wa
mazoezi. Oscar alikuwa benchi na alikuwa majeruhi”.
“Tulikuwa
na matatizo mengi, lakini wachezaji walicheza kwa kujituma na nina furaha nao.
Wameenda nyumbani na huzuni, lakini na nyuso za furaha”.
“Walifanya
kazi yao, wamepoteza mechi, lakini wamepoteza dhidi ya timu bora”. Alisema
Mourinho.
0 comments:
Post a Comment