Jose Mourinho ametozwa faini ya Pauni 10,000 kwa vurugu alizofanya kwenye mechi na Sunderland
KOCHA
Jose Mourinho amepigwa faini na FA ya England ya Pauni 10,000 kwa utovu
wa nidhamu baada ya kugombana na refa Mike Dean na mkuu wa marefa, Mike
Riley.
Mwalimu
huyo wa Chelsea, pia rufaa yake ya adhabu aliyopewa uwanja wa Villa
Park Machi imetupwa, imeelezwa amekerwa na maamuzi yote hayo.
Mourinho
aliwashambulia Dean na Riley mwezi uliopita kwa maneno kadhaa, baada ya
Sunderland kumaliza safari yake ya kucheza mechi 78 nyumbani bila
kufungwa.
Mourinho (kulia) akimzuia Msaidizi wake, Rui Faria baada ya kutolewa nje na refa Mike Dean (kushoto
0 comments:
Post a Comment