JOSE Mourinho anataka kuwaongezea mikataba wakongwe watatu wa Chelsea John Terry, Frank Lampard na Ashley Cole .
‘Mechi dhidi ya Nowrich ilikuwa ya mwisho kwa Cole, Lampard na Terry? sidhani,’ alisema Mourinho.
Katika ripoti anayotarajia kumpatia mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich, jumatatu ijayo, Mourinho anashauri kipa wa Atletico Madrid anayecheza kwa mkopo
Chelsea
Thibaut Courtois, apewe mkataba wa kudumu.
Wakongwe wa Chelsea: Jose Mourinho anataka kuwabakisha Ashley Cole, Frank Lampard na John Terry Chelsea
Hatima haijulikani: Cole, Lampard na Terry wote wanamaliza mikataba yao majira ya kiangazi mwaka huu.
Ripoti atakayokabidhi Mourinho jumatatu, imejaa mipango yake ya msimu ujao na kueleza hatima ya baadaye ya washambuliaji wake, Samuel Eto`o, Demba Ba, Fernando Torres na Romelu Lukaka anayecheza kwa mkopo Everton.
"Nimekuwa nikiandika ripoti kwa muda mrefu," alisema Mourinho. "Nitakabidhi jumatatu. Baada ya pale tutakutana ili kujadili. Napenda kuandika mapema kwasababu ndivyo napenda kufanya mambo yangu. Siku zote naandika ripoti kwa mameneja na bodi ya klabu".
"Naandika wakati msimu unaendelea na mwishoni mwa msimu nakuwa na mtazamo wangu, nachambua kila sehemu ya msimu na kila sehemu ya klabu hasa kikosi cha kwanza".
"Mimi ni kocha. Nina maoni yangu. Naijulisha klabu maoni yangu, sio maoni rahisi kama yasemwayo kwenye korido ya nyumba, nayatoa kwa njia nzuri, na napenda yatekelezwe, huwa natoa maoni kwa maandishi. Kazi yangu ni kuchambua vitu, kuwa na maoni na kufanya maamuzi yangu. Lakini huwa naheshimu mawazo ya klabu".
Kuhusu hatima ya wachezaji wawili raia wa uholanzi, Courtois na Lukaku, Mourinho aliendelea: "Sijafanya maamuzi juu ya Courtois kuhusu msimu ujao? ndiyo-lakini mimi sio klabu.
Mourinho akijibu maswali kwenye mkutano wa kabla ya mechi
"Ulikuwa msimu mzuri wa mkopo kwa Thibaut. Lukaku pia alikuwa na mafanikio katika mkopo wake".
'Wakati fulani tunawatoa wachezaji kwa mkopo, lakini mwisho wa msimu tunashindwa kueleza kwanini tuliwatoa".
'Lukaku alicheza muda wote na kila dakika ilimpatia uzoefu mzuri ndani ya timu nzuri, yenye kocha mzuri na anafunga magoli".
"Kwa hiyo amekuwa na mafaniko katika mkpo wake, na mmoja ya wachezaji wa kujitambua".
Ryan
Bertrand anaweza kuondoka Chelsea majira ya kiangazi mwaka huu baada ya mazungumzo na kocha Mourinho.
Beki huyo wa kushoto mwenye miaka 24, anataka namba ya kudumu. ‘Kuendelea Chelsea msimu ujao na kukaa benchi, sitaki," alisema Bertrand.
Anaondoka? Ryan Bertrand anaweza kuondoka Chelsea kutafuta namba ya kucheza sehemu nyinine
0 comments:
Post a Comment