KWA mara ya kwanza dunia itashuhudia fainali ya
kwanza ya UEFA mei 24 mwaka huu mjini
Lisbon, Ureno, itayozikutanisha timu mbili zinazotoka mji mmoja yaani Madrid.
Hii ni baada ya Atletico Madrid kufuzu fainali usiku
huu kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Stamford
Bridge.
Mechi ya kwanza nchini Hispania katika uwanja wa
Vicente Calderon, timu hizi zilitoka suluhu, lakini leo Chelsea wameachia na
kutolewa kwa wastani wa mabao 3-1 katika mechi zote mbili za nusu fainali.
Katika mchezo wa leo, Fernando Torres alitangulia
kuifungia Chelsea dakika ya 36 kwa pasi ya Azpilicueta baada ya kazi nzuri ya
Willian.
Dakika 8 baadaye, Adrian Lopez akaisawazishia Atletico kwa pasi ya Juanfran.
Diego Costa katika dakika ya 61 alifunga bao la pili kwa penalti iliyosababishwa na Samuel Eto`o.
Diego Costa katika dakika ya 61 alifunga bao la pili kwa penalti iliyosababishwa na Samuel Eto`o.
Wakati Chelsea wakihaha kusawazisha bao hilo,
dakika ya 72, Arda Turan alipiga kidude cha tatu na jahazi la Chelsea kutota
kabisa.
Mouringo katika dakika ya 54 alimtoa beki wake, Ashley Cole na nafasi yake kuchukuliwa na
mshambuliaji, raia wa Cameroon, Samuel Eto`o ambaye alisababisha penati
iliyowapoteza Chelsea.
Mabadiliko haya yaliwashitua wengi, lakini
Mourinho ndiye kocha na anajua kwanini alifanya mabadiliko kama hayo kwenye
mchezo muhimu kama huo.
Sasa Atletico watakutana na Real Madrid ambaojana
waliwavua ubingwa Bayern Munich kwa kuwatandika mabao 4-0, jumulisha la
Santiago Bernabeu ngoma inakuwa 5-0.
Baada ya mechi hiyo, Jose Mourinho amemsifu kipa
wa Atletico Madrid, Thibaut Courtois kwa kufanya kazi nzuri ya kulinda lango
lake.
“Mchezo kufikia muda fulani ulikuwa sawa sana,
sana, sana , sana “. Mourinho ameuambia mtandao wa Sky sports.
“Kipindi cha kwanza kilikuwa chetu kuliko wao,
lakini kumaliza 1-1 yalikuwa matokeo ya wazi. Na kipindi cha pili kiliamua kila
kitu”.
“Dakika ambayo golikipa wa Atletico aliokoa kichwa
cha John Terry nilidhani haitawezekana. Penati iliua mchezo. Sijui kama ni
penati, nilikuwa mbali sana”.
“Ilikuwa dakika muhimu kwa Atletico baada ya
kupata penati. Baada ya matokeo ya 2-1 dhidi ya Atletico nilijua sasa haiwezekani”.
“Na baada ya pale mchezo ukabaki kwa timu
iliyokuwa na morali kwani walijua wana dakika 30 tu za kumaliza mchezo na wakaamua
matokeo”. Amesema Mourinho.
0 comments:
Post a Comment