Michuano
ya mpira wa miguu wa ufukweni (beach soccer) inayoendeshwa na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikishirikisha vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam
imeingia hatua ya robo fainali.
Robo
fainali hiyo inayoshirikisha timu nane itachezwa Jumamosi (Mei 10 mwaka huu)
kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni kuanzia saa 5 asubuhi, huku Chuo
cha Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii (SWI) zikicheza robo
fainali ya kwanza.
Chuo
Kikuu cha Ardhi (AU) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere watcaheza robo
fainali ya pili kuanzia saa 6 kamili. Saa 8 kamili itaanza robo fainali ya tatu
itakayozikutanisha Taasisi ya Uhasibu (TIA) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM).
Robo
fainali ya mwisho itakayoanza saa 9 kamili itakuwa kati ya Taasisi ya
Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Utumishi Magogoni. Washindi
watacheza nusu fainali Jumapili (Mei 11 mwaka huu) kwenye ufukwe huo huo.
Mechi
za kutafuta mshindi wa tatu, na ile ya fainali zitachezwa kwenye ufukwe huo huo
wikiendi ya Mei 17 mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment