Zacharia Hans Poppe amezikaribisha klabu zenye dau nono kumendea wachezaji Simba |
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KAMATI ya usajili ya klabu ya Simba SC inatarajia
kukutana jumatatu ya wiki ijayo kujadili ripoti ya kocha mkuu, Mcroatia, Dravko
Logarusic tayari kwa mikakati ya msimu
ujao.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Keptein wa zamani wa
Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe ameuambia mtandao huu jioni hii kuwa malengo
ya Simba ni kuimarisha kikosi chao, hivyo wanaanza mikakati rasmi jumatatu kwa
kupitia mapendekezo ya Loga juu ya wachezaji atakaondelea nao na wachezaji gani
wasajiliwe.
“Tutakutana rasmi jumatatu na kufikia jumatano ya
wiki hiyo hiyo tutakuwa tumehitimisha kuijadili na kuanza harakati za kutekeleza
yaliyomo”. Alisema Poppe.
Mwanajeshi huyo wa zamani wa JWTZ aliongeza kuwa
kuna wachezaji muhimu watakaobakishwa kwasababu wana mikataba na Simba, hivyo
hakuna klabu itakayowasajili bila maridhiano na Simba sc.
“Tambwe anahusishwa kuondoka,lakini ana mkataba wa
mwaka mmoja na sisi. Kwahiyo kama mtu anataka kuzungumza naye sheria inambana
na lazima aje kuzungumza na Simba”.
“Wachezaji wote tunaohitaji kuendelea nao wana
mikataba na Simba. Kuna wengine ni mwaka mmoja, wengine miwili hadi mitatu”.
“Mfano Jonas Mkude, Ramadhan Singano wanamaliza mikataba yao 2017.
“Wachezaji wote wanaohusishwa kuihama klabu wana
mikataba mirefu na sisi”. Aliongeza Poppe.
Aidha, Poppe alisema hakuna mtu aliyeenda rasmi
kuzungumza na Simba mpaka sasa, lakini wakifika, Simba haina tatizo kwani si utaratibu
wake kuwazuia wachezaji kuondoka.
“Hata kama mchezaji yupo katika mipango ya
mwalimu, lakini timu ikataka nyingine ikahitaji kumsajili, sisi tunamruhusu na
kutafuta mwingine”.
“Ukipata dau nono unatafuta mchezaji mwingine na
unaweza kuambulia na faida kwa manufaa ya klabu”. Alisema Poppe.
Poppe aliwaondoa hofu wanachama na mashabiki wa
Simba kwasababu safari hii wanakwenda vizuri na wataanza msimu mpya kwa kasi
nzuri.
Simba sc ilimaliza msimu uliopita kwa kushika
nafasi ya 4 kwa pointi 38, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mbeya City, ya pili
Yanga na Azam fc ndio walikuwa mabingwa.
0 comments:
Post a Comment