Monday, May 12, 2014


http://api.ning.com/files/OsG-NixX39chAM-T1wK7O8cwXqJfCxg3xJGSeI2RpYKMUD09kn0WTjfWscoZf8azyhKAGd8DtDtU05In7tPa2Fs9O7-kBTZ3/simba3.jpg
Maandamano ya kumsindikiza Evans Aveva kuchukua fomu ya kugombea urais Simba sc jana. (picha na Global Publisher)

 Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
MISHEMISHE za uchaguzi wa Simba Sc utakaofanyika juni 29 mwaka huu zinaendelea kushika kasi na sasa zoezi la kuchukua fomu linaendelea.
Jana maeneo ya Msimbazi Kariokoo, jijini Dar es saaalm, makao makuu ya klabu ya Simba, mwanachama wa muda mrefu na mmoja wa waanzilishi wa Kundi la Friends of Simba (F.O.S), Evans Aveva aliteka maeneo hayo baada ya kusindikizwa na wanaosadikika kuwa wanachama wa Simba kwenda kuchukua fomu ya kugombe urais.
Kwa tulioshuhudia idadi ya watu waliomsindikiza Aveva, hakika kama kuna mtu ana nia ya kugombea urais wa Simba anaweza kugwaya.
Watu hao wanaosadikika kuwa wanachama wa Simba sc walimlaki Aveva barabara ya Lumumba na kumsindikiza kwa maandamo wakipitia barabara ya Uhuru na baadaye Msimbazi, yalipo makao makuu ya klabu yao.
Msafara huo ulizuiliwa na wahusika wa makao makuu ya klabu na kumruhusu Aveva kuingia na mtu mmoja tu kwenda kuchukua fomu, Said Tully ambaye naye alichukua fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji.
Baada ya kuchukua fomu hizo, kwa kifupi Aveva alisema mamia ya wanachama waliojitokeza wanadhihirisha nini wanakitaka kutoka kwake.
Ni ngumu kujua moja kwa moja kuwa mamia ya watu waliojitokeza ni wanachama hai wa Simba sc kwasababu hawakuonesha kadi zao na hata kama wangeonesha isingekuwa rahisi kujua kama wanazilipia.
Hata kwenye siasa za kawaida huwa inatokeo mgombea fulani anasindikizwa na kundi kubwa la wapambe wake, lakini kumbe wale watu hawana hata kadi ya kupigia kura, mwisho wa siku kura hazitoshi.
Sasa mgombe anaanza kushangaa, kwa watu wote wale walioniunga mkono, inawezekanaje sijashinda?, aaah! Lazima wamechakachua. Kumbe jamaa wapambe wake hawakuwa na vigezo vya kupiga kura.
Dalili ya mvua ni mawingu, kwa jinsi Aveva alivyoiteka Msimbazi jana, unaweza kuanza kuwaza kuwa huyu jamaa anaweza kuwa rais wa Simba sc, japokuwa ni mapema mno kuanza kuamini hayo.


IMG-20140511-WA0015Evans Aveva akichukua fomu jana makao makuu ya klabu ya Simba sc, Msimbazi Kariokoo jijini Dar es salaam


Lakini kuna wakati mtu anaweza kuwatishia wengine wenye nia ya kugombea kwa kuungwa mkono na wapambe wengi kama ilivyokuwa kwa Aveva.
Mpaka sasa ni mtu mmoja tu hadi sasa ambaye tayari amechukua fomu ya Urais mbali na Aveva, naye ni Andrew Tupa.
Ingawa hatujaona makeke ya mwanachama mwingine maarufu wa Simba sc, Michael Richard Wambura anayetarajiwa kuchukua fomu ya kugombea urais leo hii, lakini mambo ya Aveva jana ni tishio.
Wambura ni moja ya watu wanaotikisha soka la Tanzania hasa inapofika wakati wa uchaguzi. Hata kule TFF mambo huwa magumu anapoingia kwenye kinyang`anyiro. Wambura sio mgeni wa purukushani za uchaguzi. Tusubiri kuona kitakachoonekana kama kweli atajitokeza leo.
Aveva kihistoria ni mwanachama damu wa Simba na kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa miongoni mwa watu wanaoisaidia Simba kupitia kundi lao la Friends of Simba.
Hajawahi kuwa kiongozi wa kuchaguliwa, lakini amewahi kushika kamati kadhaa, na inayokumbukwa sana ni ile ya usajili mwaka 2000.
Kwa asilimia kubwa Simba iliyofanya makubwa mwaka 2003 na kuivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri yalikuwa ni matunda ya Aveva kwa kushirikiana na viongozi wenginie.
Kamati yake ilinasa vipaji vya wachezaji wakali kama vile Juma Kaseja Juma, Emmanuel Gabriel Mwakyusa, Ulimboka Mwakingwe, Boniface Pawasa, Yahya Akilimali, Suleiman Matola `Veron` na wengineo.
Kwa Simba ile iliyokuwa tishio mwa miaka hiyo, ni haki ya Aveva kusindikizwa na mamia ya wanachama wa Simba sc jana.
Kama hoja za wanachama kuamua kumuunga mkono Aveva kwa kukumbuka aliyofanya katika kamati ya usajili enzi hizo na kutaka kumrudisha kuwa rais, basi jamaa dalili zake ni nzuri kuelekea katika uchaguzi wake.


IMG-20140511-WA0013 (1)Said Tully akichukua fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji


Ni kweli Aveva anastahili heshima kwa Simba kutokana na aliyofanya nyuma, lakini sio kigezo tosha cha kusema kwa asilimia 100 anafaa kuwa Rais. Wanachama ndio wenye mamlaka na wanajua zaidi ya mtu wa nje ya Simba kuwa nani anaweza kuwa kiongozi bora.
Siku chache zilizopita niliandika kuwa wanachama wa Simba ndio wenye maamuzi ya kuchagua nani anafaa kuwa kiongozi wao mpya.
Wao ndio wanajua wapi walipatia na wapi walikosea kuchagua viongozi wao wa nyuma, hivyo juni 29 ndio siku ya kuweka mambo sawa na kurudi katika reli.
Nilisema ni ngumu sana kujua nani anafaa kuwa kiongozi kwa kuwaangalia watu machoni na uwezo wao wa kifedha.
Kiongozi bora hatokani na sura yake kuwa katika hali fulani au kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha.
Tumeshuhudia watu wenye fedha ndefu wakiongoza klabu za Simba na Yanga, lakini jiulize wameleta nini cha ziada. Hakuna maandeleo ya kujivunia zaidi ya kutambiana kwa mambo yasiyokuwa na tija kwa timu.
Timu hizi zinahitaji maendeleo kwa wakati huu, zinahitaji kujenga viwanja na akademi kwa ajili ya maandeleao ya klabu na mambo mengine kibao, lakini mara zote viongozi wanaoingia madarakani si watendaji, bali ni wanasiasa tu.
Simba kwa muda mrefu imekuwa katika hali mbaya, lakini umefika wakati wa kujipanga upya. Wanachama wanatakiwa kuwachuja watu wao vizuri, na kama wanaogombea waliwahi kuwa viongozi basi wawapime kwa yale waliyofanya siku za nyuma.
Kama Aveva atapewa urais kutokana na kazi yake aliyofanya akiwa mwenyekiti wa kamati ya usajili na kuifanya Simba kuwa tishio, basi sawa, lakini lazima wajiulize mara mbili kwasababu kuna muda historia haitakiwi kutumika kwa mambo ya msingi kwani mambo huwa yanabadilika.
Lakini kuna haja ya kuwa makini wakati huu. Lazima wachaguliwe watu makini, waadilifu, wenye nidhamu ya uongozi na si wale wanaofanya kazi kiujanjaujanja tu.
Lengo si kumfagilia yeyote, lakini wanachama wa Simba pimeni nyakati. Huu si wakati wa kufanya makosa tena, mkizembea kuna safari ya miaka mwili ili kubadilisha mambo.
Kama mnataka kurudisha heshima yenu, jengeni msingi wa viongozi bora. Epukeni wachumia tumbo.Wapo watu wanataka uongozi kwa maslahi binafsi. Hao ni hatari sana.
Mchagueni mtu kwa kuangalia uwezo wake, sera zake, uadilifu wake, hekima zake na awe na mapenzi ya dhati kuisogeza timu mbele na si kuingia na kuleta migogoro.
Huu ni wakati wa kufanya mapinduzi ili tuone mnajenga uwanja na akademi yenu.
Kila la heri Simba sc katika uchaguzi wenu. Amani na iwe nanyi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video