Sunday, May 4, 2014



 http://1.bp.blogspot.com/-7EEvxNsJ2Jo/UuU4R_-krBI/AAAAAAAA6W8/Wr3OTMedNZ8/s1600/Mess+akiwatoka+mabeki+wa+Rhino+Ragers.JPG
Na Baraka Mpenja, Dar es Salaam
0712461976
Shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza kuwa ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanzia msimu wa 2015/2016 itakuwa na timu 16 badala ya 14 za sasa.
Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mchana huu ameseme mabadiliko hayo yamepitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Mei 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo ya kuongeza idadi ya timu kutoka kwenye Kamati ya Mashindano.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa uamuzi huo umefanywa kwa lengo la kuongeza ushindani katika ligi hiyo, na kuwezesha wachezaji kupata mechi nyingi zaidi za mashindano.
Kwa mabadiliko hayo maana yake ni kuwa Ligi ya msimu wa 2015/2016 itakuwa na mechi 240 wakati kwa sasa ina mechi 182.
Mtandao huu umebahatika kukutana na makocha na wachambuzi wa soka ili kupata maoni yao, baadhi yao ni hawa hapa chini.


Ally  Mayay Tembele 
Ally Mayay Tembele ( waliochuchumaa, wa pili kushoto) enzi zake akiichezea Yanga


ALLY MAYAY TEMBELE-Beki na nahodha wa zamani wa Yanga, kwasasa kocha na mchambuzi wa soka.
Kwa upande wake amesema: “Siku zote tulitaka hivyo, tulitaka idadi ya timu za ligi kuu iongezeke sio leo wala jana”.
“Tangia mkataba wa kwanza wa Vodacom tulizungumza kwamba nia yetu ni kuwa na timu 18, mimi nilicheza ligi ya timu 18 miaka hiyo.”
“Timu 14 ni chache hakuna anayepinga hilo, binafsi napongeza mabadiliko.”
“Angalizo ni kwamba tusije tukawa ni timu zinazokuja kushiriki ligi, tupate timu zinazokuja kushindana, tupate timu kama Mbeya City fc ambazo kweli zinakuja kushindana na sio kuongeza timu zinazokuja kushiriki, hapo tutakuwa hatujafanya kitu”.
“Nashauri pia mashindano mengine yarudishwe kwasababu ni ukweli kwamba ili mchezaji awe bora, kwa mwaka anatakiwa kucheza mechi si chini ya 40 au 50”.
“Uingereza mchezaji anacheza mechi mpaka 60, hapa kwetu mchezaji anacheza mechi 26 za ligi kuu, hatuwezi kukuza kiwango cha mchezaji kwa mechi chache hizi.”



10007397_640259669373268_1623263786_nKocha Kennedy Mwaisabula (wa mbele mwenye nguo nyeusi kushoto)


KENNEDY MWAISABULA `MZAZI`- kocha wa mpira wa miguu aliyewahi kuzifundisha timu mbalimbali za ligi kuu ikiwemo Yanga sc.
Yeye amesema: “Kwanza nawapongeza TFF kwasababu ndio kilio cha watanzania wengi kwamba timu ziongezeke, tena si 16 bali zifike mpaka 20 na ndio lengo la watu wengi”.
“Ili soka la nchi likue lazima wachezaji wawe na mechi nyingi, kwahiyo naipongeza kamati ya TFF kuliona hilo, lakini bado kuna kazi ya kuongeza mpaka zifike 20”.
“Mwaka 2001 wakati nafundisha Bandari FC ya Mtwara, timu zilikuwa 24 na usafiri wa kwenda Mtwara ulikuwa unachukua zaidi ya siku tatu, lakini bado kulikuwa na ligi ya aina hiyo”.
“Leo ukitaka kwenda Mtwara inachukua siku moja, ukitaka kwenda Mwanza ni siku moja, kwahiyo nasema tunahitaji kuwa na timu 20 kama nilivyosema, lakini napongeza kwa hizo mbili zilizoongezwa kuwa 16”.
“FIFA wanakwambia ili mchezaji afikie kiwango cha juu anatakiwa kucheza mechi 40 kwa mwaka”.
“Mashandano mengine kama ligi ya muungano, Kombe la FA, kombe la Taifa yarudishwe, kama FA itakuwepo na mimi nitaingiza timu yangu ya Maji Matitu,  hahahah!”.
 minziro-jkt
 FREDY FELIX MINZIRO- Kocha wa JKT Ruvu, lakini kwa muda mrefu amefanya kazi na Yanga sc.
Kwa upande wake yeye amesema: “Kama wameongeza timu, basi na maeneo mengine kama udhamini, maamuzi vifanyiwe kazi”.
“Kuongeza timu ni jambo zuri na wachezaji watakuwa na mechi nyingi, hivyo ligi itazidi kuwa na ushindani”.
“Kila timu itakuwa imejiandaa kivyake, lakini wadhamini wa ligi kama Vodacom, Azam watatakiwa kutoa fedha kwa wakati muafaka ili timu zote zijiandae vizuri”.
“Timu zinapokuwa nyingi, mambo ya udhamini nayo yaende sambamba, wakichelewesha timu zitatofautiana kimaandalizi”.
Mtandao huu unaendelea kuzungumza na wadau na makocha wa soka mbalimbali, nini maoni yako msomaji wetu mpendwa?.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video