Thursday, May 1, 2014



Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BEKI na nahodha wa zamani wa Yanga SC, Ally Mayay Tembele amesema Azam fc wamelamba madume ya ukweli kutoka kwa Yanga kwa ajili ya michuano ya kimataifa na kutetea ubingwa wao wa ligi kuu bara msimu ujao.
Mayay ameuambia mtandao huu kuwa Azam fc wenye kibarua cha ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani wanatakiwa kusajili wachezaji wenye uzoefu ili kufanya vizuri.
“Azam kwasasa wanahitaji kusajili wachezaji wenye kiwango cha juu na uzoefu, Kavumbagu na Domayo, banafsi nadhani watawasaidia kwa kiwango kikubwa”.
“Domayo amekuwa fiti muda wote akiwa Yanga na Taifa Stars na amekuwa mzoefu na michuano ya kimataifa”.
“Unapopata mchezaji wa aina hiyo inakuwa faida kwa klabu. Naamini kocha Omog atafaidika na usajili huo”.
“Yanga itawachukua muda kupata wachezaji kama Domayo japokuwa wakitulia wanaweza kupata mbadala”.
Usajili wa Domayo amewapasua kichwa viongozi wa Yanga kwasababu nyota huyo alikuwa katika mipango ya kocha Mholanzi, Hans Van Pluijm.
Domayo alibakiwa na mwezi mmoja tu katika mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Yanga.
Jambo la kushangaza viongozi wa Yanga walizembea kumpa mkataba mwingine, jambo lililotoa mwanya kwa Azam kuinasa saini ya nyota huyo.
Hata hivyo inaaminika Azam wamempatia Domayo dau la shililingi milioni 50, wakati Yanga walikuwa na mkwanja wa milioni 40.
Pia mshahara wa Domayo amekuwa wa kutosha katika klabu ya Azam fc kuliko Yanga.
Kiungo huyo mkabaji wa kimataifa wa Tanzania, alisaini mkataba wa miaka miwili akiwa mjini Mbeya, baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili na Yanga SC, ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Ruvu miaka miwi iliyopita.

Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father’ amesema katika kuendelea kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wamepiga hatua nyingine kwa kumsaini Domayo.

“Kama unavyojua, baada ya kumaliza msimu vizuri tukiwa mabingwa wa Bara, tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu na kwa ushauri wa mwalimu wetu (Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia kazi,”alisema Father.
Taarifa zilizopo mjini kwasasa ni kuwa Azam wapo katika mawindo ya kumnasa Mbuyu Twite wa Yanga na wakati wowote bomu linaweza kulipuka endapo Yanga haitafikia makubaliano ya haraka na beki huyo kiraka.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video