Friday, May 2, 2014



 http://1.bp.blogspot.com/-Eh7TzJpd_b4/Ue_Nc7VMe_I/AAAAAAAAMqE/OpzIGbHYkgQ/s1600/Gerardo+Martino+Barcelona+Coach.jpg
KOCHA wa Barcelona, Gerardo Martino amesema kamwe tetesi zinazoendelea juu ya hatima yake haziwezi kuathiri kazi yake wakati huu akifukuzia ubingwa wa La Liga.
Barca walipoteza matumaini ya kubeba makombe matatu msimu huu mwezi uliopita baada ya kufungwa fainali ya copa del Rey na kutolewa UEFA na sasa wamebakiwa na matumaini ya ubingwa wa ligi kuu pekee.
Wakatalunya wapo nyuma pointi nne kwa vinara wa La Liga, Atletico Madrid.
Martino amekuwa katika hatari ya kupoteza kazi, huku Michael Laudrup na Roberto Martinez wakihusishwa kutwaa kibarua hicho, lakini Margentina huyo amekiri kuwa msimu huu umekuwa mgumu kwake.
“Kwasasa nafikiria mechi mbili zijazo ambazo zinaweza kuamua kama bado tutaweza kubeba taji la La Liga”. Martino amewaambia waandishi wa habari leo hii ijumaa.
“Kuhusu tetezi za kuachishwa kazi, kiukweli haziniathiri, ninachoangalia kwasasa ni matokeo, majina ya watu wa kunirithi nayasikia, lakini hayaniathiri”.
“Mimi na klabu hatujakaa kuzungumza lolote, hakuna haja ya kuniuliza kama nitaendelea kuwepo kwasababu mkataba wangu bado ni hai sana”.
Wakatalunya kesho jumamosi wanavaana na Getafe, lakini Martino hajaathiriwa na tetesi zinazomkabili kwa sasa.
“Ni kweli Getafe wanapigana kupata nafasi nzuri, lakini klabu zote zinapigana kupata kitu fulani. Tutacheza vizuri, sio mchezo wa kesho tu bali ni mechi zote zilizosalia kumaliza msimu”.
Elche na vinara Atletico ndio wapinzani wa Barcelona katika mechi zao mbili za mwisho.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video