Thursday, May 1, 2014



KOCHA wa Everton, Roberto Martinez amekanusha taarifa kuwa klabu yake ina mpango wa kuwaachia Manchester City katika mchezo wao wa jamamosi wiki hii ili kuwanyima nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini England wapinzani wao wa jadi, Liverpool msimu huu.

Taarifa zilizozagaa kwa sasa zinaeleza kuwa mashabiki wa Everton watakuwa na furaha kama klabu yao itafungwa na vijana wa Manuel Pellegrini ili kuwanyima ubingwa mahasimu wao wa Merseyside ambao kwa miaka 24 wamekuwa katika ukame wa mataji.

Lakini Martinez amekanusha na kusema wachezaji wake hawawezi kushawishika kirahisi na watajitahidi kwa uwezo wao wote kuwafunga Man City, ikizingatiwa bado wana matumaini finyu ya kufuzu UEFA mwakani.

“Sina wasiwasi na klabu yangu katika mashindano ya ligi. Sisi ni klabu ya mpira wa miguu na tunahitaji kushinda kila mchezo uliopo mbele yetu”

“Kuiachia timu nyingine” hapana! Huwa hatufanyi kazi kama hiyo. Tutajitahidi kushinda kila mchezo na tuko katika kiwango kizuri. Tunaiwakilisha vizuri klabu yetu”.

“”Kamwe hatutaweza kumzawadia mtu ushindi. Hatuibebi klabu yoyote”.

Kocha huyo wa zamani wa Wigan pia ameeleza kuwa mchezaji wake Phil Jagielka atajumuishwa katika kikosi cha jumamosi, wakati Sylvain Distin naye atakuwa tayari kurudi uwanjani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video