Marouane Fellaini amekuwa na msimu mgumu sana Manchester United akitokea Everton.
KIUNGO wa Manchester United, Marouane
Fellaini amesema majeruhi aliyokuwa nayo yamemfanya awe na kiwango kibovu, lakini ameahidi kufanya vizuri msimu ujao.
Fellaini
alisajili siku ya mwisho ya usajili kutoka Everton kwa ada ya uhamisho
wa paundi milioni 27, lakini ameshindwa kuonesha thamani yake na
kuisaidia United kutetea ubingwa na kufuzu UEFA
Kiungo
huyo aliumia mkono wake wakati wa mechi ya UEFA hdidi ya
Shakhtar Donetsk katika mchezo wake wa tatu tangu ajiunge na United na
alilifanyiwa upasuaji mwezi desemba mwaka jana na kukaa nje ya uwanja
moaka mwezi februari.
Ataimarika: Kiungo huyo raia wa Ubelgiji amesema atarudi kwenye kiwango chake msimu ujao
Nyota huyo ataitumikia timu yake ya Taifa ya Ubelgiji katika mechi za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu.
Fellaini aliwaambia Daily Telegraph:
'Nahitaji kuwa fiti ili niwe mzuri. Nimekuwa nikicheza hata kama nina majeruhi, lakini siko fiti. Niliumia kwa miezi mitatu na imekuwa wakati mgumu kwangu".
"Baada ya kumalizika kwa msimu huu nitaanza kujiandaa na msimu ujao na nadhani utakuwa mzuri".
Fellaini anasema David Moyes ni kocha mzuri na atarudi kazini muda si mrefu
Kwa misimu mitano akiwa Goodison Park, Fellain alikuwa mchezaji muhimu.
0 comments:
Post a Comment