Kiongozi wa msafara wa Timu ya Malawi Mrs Flora Mwandira akiongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya |
Mwalimu wa timu hiyo Young Chimodzi |
Timu
ya Taifa ya Malawi imefurahishwa na mapokezi mazuri waliyoyapata Mkoani
Mbeya na kuahidi kuonesha kandanda safi kati yake na timu ya
Taifa (Taifa stars).
Kauli
hiyo imetolewa na Kiongozi wa msafara huo Mrs Flora Mwandira na kuungwa
mkono na Mwalimu mkuu wa timu hiyo Young Chimodzi aliyewahi kuichezea
timu ya Taifa ya Malawi kwa miaka kadhaa.
Mwandira
amesema Timu ya Malawi imewasili na msafara wa wachezaji 20 na viongozi
12 ambao waliwasili siku ya alhamisi jioni na kufanya mazoezi katika
uwanja wa Sokoine.
Mchezo
huo umevuta hisia za watu wengi umevuta hisia za wakazi wa Jiji la
Mbeya na Mikoa ya Jirani na kufanya nyumba nyingi za wageni kujaa.
Mwalimu
wa timu hiyo ameweka hadharani wachezaji waliwasili kupambana na Taifa
Stars kuwa ni Makipa Charles Swin na Richard Chipuwa na Walinzi Pirilani
Zonda,Francis Mulimbika,John Lanjesi,Emmanuel Zoya,Bashiri Maunde na
George Nyirenda.
Wachezaji
wa kiungo ni pamoja na John Banda,Mecium Mhone,Douglas Chirambo,World
Nkuliwa,Frank Banda,Junior Chimodzi,Phillip Masiye na Ndaziona
Chatsalira.
Washambuliaji ni Gaston Simukonda,Green Harawa,Diverson Mlozi na Rodrick Gonani.
Kwa
upande wa chama cha mpira nchini kimetangaza kuwa kiingilio katika
mchezo huo kitakuwa ni shilingi 5000 na hakuna magari yatakayo ruhusiwa
kuingia uwanjani isipokuwa magari ya wachezaji,Polisi na Gari la
wagonjwa na tiketi zitaanza kuuzwa saa mbili asubuhi siku ya Jumapili
katika vituo mbali mbali Jijini Mbeya.
Katibu
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya(MREFA)Seleman Harubu
amewataka washabiki kufika kwa uwingi uwanjani na kuishangilia timu yao
ya Taifa kwa amani na utulivu ili kuenzi heshima iliyopewa Mkoa wa Mbeya
kwa TFF kukubali mchezo huo kufanyika Mkoani hapa.
Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment