Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MAMBO yaiva!.
Kamati ya uchaguzi ya Simba imepanga uchaguzi mkuu wa klabu hiyo kufanyika juni
29 mwaka huu baada ya msajili wa vyama vya michezo na klabu kuipitisha katiba
yao iliyofanyiwa marekebisho.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu
ya Simba yalipopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo, jijini Dar es salaam leo mchana,
mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba sc, mwanasheria na wakala wa
wachezaji wa FIFA, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kamati yake imekutana jana na
kuamua tarehe hiyo ya uchaguzi ili kupata rais mpya, makamu wa rais na wajumbe
wapya wa kamati ya utendaji.
“Kamati yangu ina
watu makini na wenye uadilifu mkubwa. Pia wana mawazo ya kuijenga klabu ya
Simba”.
“Jana tulikutana
na kupanga ratiba ya uchaguzi. Hatutakuwa na huruma na watu watakaoenda kinyume
na kanuni za uchaguzi”. Alisema Ndumbaro.
Ndumbaro alisema
kuanzia mei 9 mwaka huu mchakato wa kuanza kutoa fomu kwa watu wenye nia ya kuwania
nafasi za uongozi utaanza rasmi, na siku ya kurudisha fomu ni mei 14 mwaka huu.
Ismail Aden Rage safari yake yaelekea ukingoni Simba sc |
Mei 17 mwaka huu
kamati ya uchaguzi itafanya zoezi la kuhakiki fomu za wagombea wa nafasi
mbalimbali ndani ya klabu ya Simba.
Aidha, Ndumbaro
aliongeza kuwa mei 19 mwaka huu kamati yake itatangaza majina ya wagombea na
mei 20 watafungua milango ya pingamizi dhidi ya wagombea.
Mei 25 mwaka huu
kamati ya uchaguzi itaanza kusikiliza pingamizi na mei 27 zoezi la usaili wa
wagombe litaanza.
Mei 29 kamati ya
uchaguzi ya Simba itatangaza matokoe ya usaili na mei 30 masuala ya maadili
yataangaliwa.
Baada ya zoezi
hilo, Ndumbaro alisema juni 2-9 mwaka huu zoezi likalofanyika ni kukata rufaa kamati
ya rufaa na juni 10-12 rufaa zitasikilizwa.
Juni 16, 2014
zoezi litakuwa ni kukata rufaa kamati ya rufaa ya maadili, na juni 16-20 maamuzi
ya mwisho ya kamati ya rufaa na kamati ya rufaa ya maadili yatafanywa.
Baada ya hapo
juni 21 orodha ya mwisho ya wagombe itatangazwa na juni 24-28 kampeni za kunadi
sera kwa wagombe zitaanza.
Juni 29 ni siku
ya uchaguzi ambapo Simba itapata rais mpya atayerithi mikoba ya mpiganaji Ismail
Aden Rage.
Hii itakuwa siku muhimu sana kwa wana Simba
wote na wanachama ndio wenye mamlaka ya kuamua nani aiongoze klabu hiyo baada
ya sinema nyingi kuonekana katika uongozi wa Rage.
Rage amekuwa akilaumiwa kwa muda mrefu na
baadhi ya wanachama wa Simba kwa madai kuwa ameshindwa kukidhi matarajio yao,
lakini sasa safari yake iko ukiongoni.
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya viongozi na
timu kufanya vizuri uwanjani, bila shaka wanachama mtachagu viongozi wazuri.
Safar njema kwa Simba kuelekea katika uchaguzi
wenu. Amani itawale kwa muda wote.
0 comments:
Post a Comment