Mamadou Sakho akimuangusha Daniel Sturridge wakati wa mazoezi ya Liverpool.
ALMANUSURA beki wa Liverpool, Mamadou
Sakho ailetee janga klabu yake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya
Newcastle baada ya kumfanyia rafu mbaya mshambuliaji wa klabu hiyo
Daniel Sturridge wakati wa mazoezi leo.
Sakho
alikuwa sehemu ya ulinzi kwenye sare ya 3-3 dhidi ya Crystal Palace
jumatatu ya wiki hii, ambapo Liverpool walianza kuongoza kwa mabao 3-0
mpaka dakika ya 79.
Wakiwa
katika mazoezi hayo yaliyofanyika uwanja wa Melwood, beki huyo alikuwa
anakaba kama anacheza mechi na alimuangusha Sturridge, lakini kwa
bahati nzuri mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England hakuumia.
Mshambuliaji huyo alionekana kukosa furaha baada ya kuangushwa na Sakho
Kocha wa Liverpool , Brendan Rodgers bado anaamini kuwa klabu yake inayo nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini England.
Siku ya furaha: Kocha Brendan Rodgers na wachezaji wake walionekana wakiwa na furaha leo katika uwanja wa Melwood
0 comments:
Post a Comment