Na Baraka Mpenja, Dar es
salaam
WAPENZI wa soka jijini Mbeya wanatarajia kuishuhudia timu yao ya
taifa ya Tanzania, Taifa stars kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini
humo, aprili 4 mwaka huu ikicheza na
Malawi katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.
Hii itakuwa mechi ya pili kwa Stars ya maboresho katika harakati
zake za kujipima ubavu kabla ya kuanza kampeni za kuwania kufuzu fainali za
mataifa ya Afrika, AFCON zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Aprili 26 mwaka huu, siku
ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Taifa stars
iliyosheheni wachezaji waliopatikana katika mpango wa maboresho ya Taifa stars
ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi na kulala mabao 3-0.
Hii itakuwa ni mechi ya kwanza kwa kocha mpya wa Stars Mart
Nooij kuiongoza Stars katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi, kaimu kocha mkuu, Salum
Madadi ndiye aliyekalia benchi , huku Nooij akiwa jukwaani kutazama vipaji.
Baada
ya kuitazama Stars ikizama kwa Burundi, Mart Nooij aliongeza wachezaji tisa
katika kikosi hicho
Wachezaji
walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu Shooting),
Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday
(Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (AC
Cannes, Ufaransa).
Taarifa iliyotumwa na afisa habari wa TFF, Boniface Wambura
Mgoyo kwa vyombo vya habari jioni hii inaelezwa kuwa timu ya Taifa ya Malawi
(Flames) imewasili jijini Mbeya tayari kwa mechi ya kirafiki hiyo ya jumapili.
Wambura alisema Malawi imewasili jana (mei 1 mwaka huu) saa 1
jioni kwa njia ya barabara ikiwa na msafara wa watu 31 na imefikia hoteli ya
Manyanya.
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo
jijini Mbeya tangu Aprili 27 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.
Wambura ametaja Kiingilio katika mechi hiyo kuwa ni sh. 5,000
wakati tiketi zitauzwa siku ya mchezo kuanzia saa 2 asubuhi katika vituo vya
Uyole, Mwanjelwa,, Mbalizi, Stendi Kuu, Holiday Inn na Uwanja wa Sokoine.
Magari yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni ya wachezaji, gari
la wagonjwa, gari la zimamoto na gari la waamuzi pekee.
Taifa
Stars imepangiwa kucheza na Zimbabwe katika raundi ya pili ya mechi za mchujo
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani
nchini Morocco.
Stars
itaanzia nyumbani ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Mei 16 na 18 wakati
ile ya marudiano itachezwa Harare kati ya Mei 30 na Juni 1 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment