Makocha wa timu za Tanzania (Ngorongoro Heroes), John Simkoko na Nigeria (Flying Eagles), Manu Garba wanakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mikakati yao kwa ajili ya mechi ya Jumapili.
Mkutano huo utafanyika kesho (Mei
10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kuanzia saa 5 kamili asubuhi.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya
pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20
itafanyika Jumapili (Mei 11 mwaka huu) saa 10 kamili jioni katika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Fainali hizo za 19 za Afrika
zitafanyika mwakani nchini Senegal zikishirikisha timu saba zitakazofuzu
kwenye mechi za mchujo, na Senegal wanaoingia moja kwa moja kutokana na
kuwa wenyeji.
Wakati Ngorongoro Heroes leo (Mei
9 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi yake Uwanja wa Azam uliopo
Chamazi, Flying Eagles yenyewe muda huo huo itafanya mazoezi Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume.
Viingilio katika mechi hiyo ni
sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa sh. 5,000. Tiketi
zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika magari maalumu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment