KOCHA wa zamani wa Manchester United, David Moyes ameoenaka tena mtaani ijumaa usiku baada ya kutembelea Glasgow kwa ajili ya kunyoa nywele.
Kocha huyo wa zamani wa mashetani wekundu alitimuliwa kazi mwezi uliopita na ameenda kunyoa nywele katika saluni maarufu ya five-star Taylor Ferguson katika mji wa Scottish.
Moyes hakufanya vizuri katika msimu wake wa majanga Old Trafford , lakini leo aliweza kupiga picha na mmiliki wa saluni hiyo.
Ferguson ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuhusu kutembelewa na Moyes na kusema: " ni vizuri kumkaribisha katika saluni, David Moyes leo hii"
Ryan
Giggs aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda baada ya Moyes kuondoka, lakini United wanatarajia kumtangaza Mholanzi, Louis van Gaal kuwa kocha mkuu mpya.
0 comments:
Post a Comment