Uongozi
wa klabu ya Young Africans Sports Club umeitisha mkutano mkuu wa
wanachama wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama waweze kutoa maamuzi
kwenye baadhi ya vipengele vilivyoongezwa kabla ya kuelekea kwenye
mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa viongozi.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani,
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema wamefikia kuitisha
mkutano huo wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama wapate fursa ya
kupitisha baadhi ya vipengele kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
"Tumekua
na mawasiliano na TFF juu ya kuongezwa baadhi ya vipengele kwenye
Katiba yetu kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi, baada ya hapo ni
nafasi kwa wanachama wa Yanga sasa kukutana na kuweza kupitisha hivyo
vipengele vitakavyoongezwa kwenye Katiba Mpya" alsiema Beno.
Aidha
Beno amesema wanachama wakishapitisha/kukubaliana juu ya hivyo
vipengele ndipo uoungozi utawasilisha mapendekezo hayo kwa TFF ambayo
ikishayabariki, yatapelekewa kwa Msajili nae akiyapitisha ndipo itakua
tayari ni Katiba halali ambayo itatumika kwwenye uchaguzi mkuu.
"Nawaomba
wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano wa mabadiliko
juni mosi 2014 ili waweze kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea
kuwa na Katiba Mpya itakayotumika kwa shughuli za kila siku za klabu
ya Yanga SC" aliongea Beno.
Eneo na Ukumbi utakapofanyika mkutano huo Juni Mosi 2014 utatangazwa hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika.
Chanzo: Tovuti ya Yanga
Chanzo: Tovuti ya Yanga
0 comments:
Post a Comment