LIVERPOOL wanahangaika kumbakiza mshambuliaji wao Luis Suarez majira ya kiangazi mwaka huu.
Inafahamika kuwa Real Madrid au Barcelona zipo mbioni kuiwania saini ya nyota huyo raia wa Uruguay.
Suarez alisaini mkataba mrefu katika klabu ya Liverpool miezi minne iliyopita, lakini haimzuii kuondoka.
Anawindwa: Real Madrid na Barcelona wanatarajia kupambana kuinasa saini ya mshambuliaji hatari wa Liverpool, Luis Suare.
Inafahamika kuwa Suarez anaweza kuondoka kwa dau la Uro milioni 100 sawa a paundi milioni 82.
Real Madrid ndiyo timu yenye nia kubwa kumsajili, lakini Barcelona wanaweza kuingia katika vita hiyo.
Kwa upande wa Suarez ndoto yake ni kucheza Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment