NGORONGORO HEROES YAPIGWA 2-0 NA NIGERIA TAIFA
FT: NGORONGORO HEROES 0 : 2 NIGERIA
Dakika 45` za kipindi cha pili zimemalizika ka kuongezwa dakika 3` za nyongeza.
Kelvin Friday anajituma kupiga krosi lakini washambuliaji wa kati Juma Luizio na Saady Kipanga wanashindwa kufanya kazi nzuri.
Dakika ya 41` kipindi cha pili Nigeria wanaongoza kwa mabao 2-0.
Dakika ya 40` kipindi cha pili, Ngorongoro wapo nyuma kwa mabao 2-0.
Dakika ya 37` kipindi cha pili Nigeria wanaandika bao la pili.
Dakika ya 30` kipindi cha pili Nigeria wanaongoza kwa bao 1-0
Dakika ya 29` kipindi cha pili Nigeria wanapiga kona haizai matunda
Dakika ya 27` kipindi cha pili Nigeria wanapata kona.
Nigeria wameshakubali kuchezewa mpira, lakini vijana wa Ngorongoro wanakosa maarifa ya kufunga.
Dakika hizi Ngorongoro wamecharuka, lakini mabeki wa Nigeria wapo imara bado.
Dakika ya 22` kipindi cha pili Kelvin Friday anaingiza krosi nzuri na inampita kipa wa Nigeria, lakini hakuna wa kumalizia.
Dakika ya 21` Ngorongoro wanafanya shambulizi kali, lakini kichwa cha Saady Kipanga kikawa hakina nguvu na kipa akaokoa.
Dakika ya 20` kipindi cha pili Ngorongoro wanapata kona haizai matunda.
Dakika ya 16` kipindi cha pili Nigeria bado wanaongoza kwa bao 1-0.
Kelvin Friday anatandika shuti lakini linapaa juu ya lango.
Dakika ya 10` kipindi cha pili Nigeria bado wanaongoza kwa goli moja kwa bila.
Dakika ya 8` kipindi cha pili Nigeria wanafanya shambulizi kali, lakini kipa Peter Manyika anaokoa na kuwa kona, haijazaa matunda.
Dakika 3` kipindi cha pili Nigeria wanaandika bao la kuongoza baada ya Yahaya Musa kumalizia krosi ya Mohamed Musa.
Kipindi cha pili kimeshaanza hapa uwanja wa Taifa.
Kipa wa akiba Peter Manyika anaingia kuchukua nafasi ya Aishi Manula aliyeumia
Juma Luizio Ndanda anataka kuingia kuchukua nafasi ya Gadiel Michael.
Dakika 45` za kipindi cha pili kitaanza hivi punde, waamuzi wanakagua nyavu
..........................................................
Kwa ujumla dakika 45` zimeenda vizuri kwa Heroes, lakini vijana wamekosa uchangamfu. Kuumia kwa Manula ni tatizo kwa timu ya Taifa. Kikubwa vijana wanahitaji kuwa makini kutumia nafasi wanazopata. Ngorongoro wamepata nafasi za kufunga, lakini tatizo la umaliziaji ni kubwa sana.
HT: NGORONGORO HEROES 0 : 1 NIGERIA
Dakika 45` za kipindi cha kwanza zimeshakatika na zinaongozwa dakika 4`
Dakika ya 40` kipindi cha kwazna hakuna bao lolote.
Dakika ya 30` kipindi cha kwanza golikipa wa Ngorongoro Heroes Aishi Manula yupo chini anagangwagangwa baada ya kupata mshikeli.
Dakika ya 29` kipindi cha kwanza milango bado ni migumu
Dakika ya 20` kipindi cha kwanza hakuna goli lolote
Dakika ya 5` kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa.
NGORONGORO HEROES 0 VS 2 NIGERIA
0 comments:
Post a Comment