
Na Braka Mpenja, Dar es salaam
CHAMA cha soka visiwani Zanzibar, ZFA kimebainisha
kuwa ukosefu wa udhamini mnono kwenye michuano ya ligi kuu Zanzibar kumeifanya isiwe na mvuto kama ilivyo kwa
Tanzania bara.
Katibu mkuu wa ZFA, Masud Ettei ameuambia mtandao
huu kuwa ligi kuu ya Zanzibar ina mdhamani mmoja tu ambaye ni Grand Malta,
wakati huo huo klabu zinazoshiriki ligi hiyo hazina udhamini.
“Tunashukuru tunachokipata kwa mdhamini wetu,
lakini anachotoa hakiwezi kukidhi mahitaji ya ZDF”
“Tungekuwa na udhamini mzuri tungekuwa bora kama
ilivyo kwa Tanzania bara”.
“Unajua ZFA imetafuta mdhamini ambaye ni TBL chini
ya kinywaji chake cha Grand Malta,
lakini timu zenyewe zimekosa udhamini kama vile Simba na Yanga ambazo mbali na wadhamini
wa ligi Vodacom na Azam TV , pia wana
udhamini wa TBL”.
“Angalia Azam TV walivyoamua kuwekeza udhamini wao
katika ligi, hii imeongeza chachu, hivyo nasisi Zanzibar tungetamani kuona
udhamini kama huu”. Alisema Masud.
Masud ameomba makampuni mbalimbali kujitokeza
kudhamini ligi ya Zanzibar pamoja na klabu zinazoshiriki ligi hiyi ili iendane na kasi ya soka la kisasa.
“Klabu zikisaidiwa kwa udhamini, zitaweza kufanya
maandalizi mazuri, zitalipa mishahara na posho kwa wachezaji kwa muda muafaka
na kuinua hamasa”.
Aidha, Masud alisema Zanzibar ina wachezaji wazuri
sana hasa vijana, lakini kukosekana kwa udhamini inawaumiza kichwa mno.
“Bara wenzetu wana michuano ya vijana kama Uhai
Cup, lakini kwetu hakuna mashindano ya vijana. Tunao vijana wenye vipaji,
lakini hatuna uwezo wa kuendesha mashindano”.
“Tunapendekeza makampuni yaje kutusaidia nasisi
turudi katika kiwango cha juu kama ilivyo kwa wenzetu wa bara”. Aliongeza
Masud.
0 comments:
Post a Comment