Na Mwandishi wetu
Mlinzi kiraka wa timu ya Young Africans Mbuyu Junior Twite leo ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga baada ya kufikia makubaliano na uongozi na kupata majibu ya Shirikisho la Soka nchini TFF juu ya idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa msimu ujao 2014/2015.

Usajili
wa Twite umefanyika leo makao makuu ya klabu ya Yanga chini ya Katibu Mkuu Bw
Beno Njovu ambapo mchezaji amesema ataendelea kujitolea kwa uwezo wake
kuisaidia timu yake ya Yanga.
Katibu
Mkuu wa Young Africans Beno Njovu amesema wameingia mkataba wa mwaka mmoja na
Twite baada ya pande zote kukubaliana, hivyo kuanzia sasa Twite ataendelea kuwa
mchezaji wetu kwa msimu ujao wa 2014/2015 na kusisitiza kuwa usajili ndio
umeanza sasa.
Akiongea
mara baada ya kuweka sahihi kwenye mkataba wake mpya Twite amesema anajisikia
furaha kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga, kwani anafurahia maisha ya Jangwani,
wapenzi, washabiki, viongozi na wachezaji ni marafiki/ndugu ndani na nje ya
Uwanja.
Aidha
Twite amesema Yanga ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, zenye washabiki
na waachama wengi hivyo wangu ni fahari kuendelea kuitumika timu hii ambayo
tangu kujiunga nayo nimekua nikijtoa kwa moyo wangu wote kusaka
mafanikio.
Mbuyu
Twite amekua ni mchezaji wa Young Africans kwa kipindi cha miaka miwili tangu
Julai 2012 alposajiliwa huku katika kipindi hicho chote akiwa ni mchezaji wa
kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliweza kuisadia timu yake kutwaa
Ubingwa wa Lig Kuu ya Vodacom na msimu huu kushika nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment