Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MCHAKATO wa maboresho ya timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa stars uliohusisha makocha mbalimbali kuzunguka mikoani kwa
lengo la kung`amua vipaji vilivyofichika
umeendelea kukosolewa na baadhi ya wataalamu wa soka.
Akizungumza na mtandao huu, kocha msaidizi wa
Mbeya City fc, Maka Mwalwisyi amesikitishwa
sana na shirikisho la soka Tanzania TFF, kuamua kutumia mfumo huu badala ya
kuhangaika kujenga msingi wa soka ambao ndio kilio cha watanzania wengi.
Maka alisema watanzania kwasasa hawahitaji kuona
TFF inahangaika na timu ya Taifa kwa kutafuta wachezaji wasiocheza ligi kuu, kwasababu
kupata mafanikio kwa mfumo wa sasa ni ngumu sana na hata mataifa makubwa
hayawezi kutengeneza timu ya taifa inayojiandaa na mashindanio mwaka mmoja
mbele kwa mfumo huu.
“Mimi nashangaa sana na nitaendelea kushangaa,
kwanini makocha walipitisha mpango huu?, hivi kama kweli mchezaji yupo Mbeya na
ana kiwango cha juu, sisi Mbeya City tutashindwa kumuona kweli? Hata wenzetu
Prisons wasimuone, hapana”.
‘Wanachagua makocha kuzunguka nchi nzima na
kutumia fedha nyingi, sidhani kama ni suluhisho, kuna mambo mengi ya kuyafanya
hasa kujenga misingi ya soka la vijana”.
“Mchezajai hachezi ligi, unamchukua kutoka
mchangani na kumleta Taifa stars, halafu unawadanganya watanzania kuwa unataka
uipeleke timu AFCON mwakani nchini Morocco”.
‘Hivi huyu mchezaji ambaye hachezi ligi, itakuwaje
akikutana na wachezaji wanaoshindia mpira kama magharibi mwa Afrika?, hivi ni
vichekesho tu”. Alisema Maka.
Kocha huyo aliongeza kuwa TFF wangeshauriwa
kuendeleza timu ya `Young Future Taifa stars` iliyoanzishwa na kocha
aliyevunjiwa mkataba, Mdenish Kim Poulsen kwasababu ilijumuisha wachezaji wa
ligi kuu.
“Kim alikuja na mpango mzuri, lakini wameona kama
haufai”.
“ Ile timu ya Young Future Taifa stars ndio
ingewekwa kambini miezi miwili Tukuyu, angalau tungepata watu fulani”
“ Lakini kwa kikosi chao kile cha maboresho,
hawajafanya kitu pale na nashukuru watanzania kugundua hilo kwasababu nawasikia
wakisema”.
“Nadhani kocha Mart Nooij aliwaambia kuhusu wachezaji
hawa. Niliwaona na kugundua kuwa hawana msaada kwa Stars. Ndio maana
hawakupangwa hata kwenye mechi dhidi ya Malawi”.
“Rais Malinzi na watu wake wakae chini tena
kuufikiria mfumo huu. Nadhani si busara kuacha kila lililokuwa linafanywa na
watu wa nyuma”.
“Mazuri yaendelezwe na mabaya yasahihishwe ,
lakini kwa mwendo huu nakuw a na mashaka”.
‘Unashindwa kuchukua wachezaji kutoka Mbeya City
fc iliyomaliza nafasi ya tatu”
“ Unakwenda kutafuta watu wasiojulikana kwa
kutumia fedha nyingi na hawachezi ligi, hakika unaleta utani tu”. Alimaliza
Maka.
0 comments:
Post a Comment