Kazini: Mfungaji wa bao la kwanza la Liverpool jumatatu ya wiki hii, Joe Allen (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Palace, Marouane Chamakh
Ajabu: Gayle akishangilia na Yannick Bolasie, baada ya kuchafua hali ya hewa kwa Liverpool uwanja wa Selhurst Park
Manyoya
tu: Kipa wa Palace, Julian Speroni akishindwa kuokoa mpira uliopigwa na
Daniel Sturridge na kuifungia Liverpool bao la pili.
Suarez akishangilia kufikia rekodi ya Alan Shearer na Cristiano Ronaldo ya mabao 31 kwa msimu mmoja, lakini timu yake ilitoka sare ya 3-3 na kumwaga machozi baadaye.
Brendan Rodgers |
KOCHA
Liverpool, Brendan Rodgers bado hajakata tamaa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu
soka nchini England licha ya kuharibiwa na Crystal Palace jumatatu ya wiki.
Mabao
ya Damien Delaney na Dwight Gayle katika dakika 11 za mwisho yalipunguza kasi ya
Liverpool na kutoka sare ya 3-3, hivyo kuwafanya Manchester City wawe na
asilimia kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa.
Rodgers
ambaye timu yake ipo kileleni kwa pointi moja mbele lakini wakiwa na mchezo
mmoja zaidi ya Man City alisema Liverpool itaendelea kupigana mpaka mwisho wa
msimu, licha ya wengi kuamini mbio za ubingwa ziliisha jumatatu.
“Wachezaji
bado wapo katika morali na wamewaomba mashabiki wao kutofuta ndoto za ubingwa”.
Alisema.
“Kuwa
na timu ambayo ipo mbele kileleni kwa pointi moja huku tukiwa na wiki moja ya
kwenda ni jambo zuri”
“Huwezi
kujua nini kitatokea, sisi tutajituma mpaka mwisho”.
“Ninachoweza
kuahidi ni kuwa, kwa vile nipo hapa, timu itapigana kufa na kupona. Msimu
haujaisha mpaka mechi yetu na Newcastle”.
Rodgers
amewashukuru wamiliki wa timu kwa kuwa na imani kubwa na yeye na kuna taarifa
kuwa atapewa mkataba mpya.
“Napenda
kuwashukuru wamiliki na mkurugenzi wa timu kwa kile wanachonifanyia tangu
nimefika hapa.” Rodgers alisema.
“Walimleta
kocha kijana mwenye miaka 39 katika moja ya klabu kubwa duniani na kunipa
nafasi ya kujiendeleza katika falsafa yangu ya mpira”.
“Kama
sio imani yao kwangu, yawezekana nisingekuwepo hapa ukizingatia uhalisia wa
soka la kisasa”.
0 comments:
Post a Comment