JURGEN
Klopp amesema Marco Reus atakuwa mfungaji bora msimu ujao na kuziba pengo la
Robert Lewandowski anayejiandaa kuondoka Borussia Dortmund majira ya kiangazi
mwaka huu.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Poland alimaliza akiwa mfungaji bora wa Bundesliga kwa
mabao 20 na anajiandaa kuondoka katika klabu yake kujiunga na wapinzani wakubwa
wa Dortmund, Bayern Munich.
Klopp
hana wasiwasi wa kumpoteza mshambuliaji huyo mwenye miaka 25 na amesisitiza
kuwa Reus aliyefunga mabao 16 katika mechi za ligi atachukua majukumu ya
Mpoland huyo.
“Msimu
ujao ni muda wa Reus kumaliza msimu wa Bundesliga akiwa mfungaji bora,” Klopp
aliwaambia waandishi wa habari baada ya ushindi wa mabao 4-0 jana jumamosi.
Reus
alipata majeruhi jana na nafasi yake kuchukuliwa na Pierre-Americk Aubameyang,
lakini klabu kupitia tovuti yake imesema kuwa nyota huyo mwenye miaka 24 hayuko
hatarini kukosa mechi ya fainali ya DFB-Pokal dhidi ya Bayern Munich jumamosi
ijayo.
0 comments:
Post a Comment