Thursday, May 1, 2014



 article-2617143-1D7BCD8D00000578-458_634x415
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa,  ameitandika Chelsea  bila huruma na kuisaidia klabu yake kufuzu fainali licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa atajiunga na Chelsea majira ya kiangazi mwaka huu.
Costa alifunga bao la penati na katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea na kumfanya Diego Simeone akutane na Carlo Ancelotti katika mchezo wa fainali mjini Lisbon nchini Ureno mwezi ujao.
Mtandao huu kupita mtandao rafiki wa Goal.com unafahamu kuwa Chelsea wametenga kitita cha pauni milioni 35 kukamilisha usajili wa nyota huyo mwenye miaka 25.
Costa amekiri kuwa kwasasa hajaamua maisha yake ya baadaye.
“Kucheza Chelsea baadaye? Tutaona, najua kuna ofa kwa ajili yangu, najisikia vizuri kuwepo Atletico” ameuambia mtandao wa Sky Italy.
Adrian Lopez na Arda Turan pia walifunga, lakini Chelsea walikuwa wa kwanza kufumania nyavu za Atletico kupitia Fernando Torres.
Costa ameuelezea mchezo wa leo kuwa ni “wa maajabu na historia” na amemsifu kocha wake Diego Simeone kuifanya Atletico kuwa na makali zaidi msimu huu.
“Ni kitu cha ajabu na kihistoria. Tumejituma kwa nguvu zote kufika fainali hii”. Costa amezungumza na Canal Plus.
“Mpira haukuishia kwenye penati tu, lakini ulimalizika vizuri. Nadhani timu inafanya vitu sahihi, lakini Diego Simeone amefanikiwa kufanya maamuzi sahihi kila wakati”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video