KIUNGO wa Coastal Union, Mkenya Jerry Santo
anataka kurudi Simba sc msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara, mtandao wa Goal.com umeandika.
Santo kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba
wake wa miaka miwili katika klabu ya Coastal Union kumalizika msimu huu.
Kiungo huyo siku za nyuma aliichezea Simba baada
ya kujiunga nayo kutokea Tusker ya Kenya mwaka 2009.
Santo alishinda taji la Kenya akiwa na Tusker
mwaka 2006 na mwaka 2009 aliteuliwa kuwa nahodha katika misimu yake mitatu
klabuni hapo.
Santo ameuambia mtandao wa Goal.com kuwa hayuko tayari kuongeza mkataba na Coastal, kwasababu hana furaha na mazingira ya timu
hiyo iliyomaliza msimu katika nafasi ya 8.
“Mazingira yaa Coastal
Union sio mazuri kwa upande wangu, lakini sasa nataka kurudi Simba ambako
nilicheza kwa mafanikio makubwa na kurudi timu yangu ya Taifa, `Harambee
Stars`, alisema Santo katika mahojiano maalum na Goal.com
0 comments:
Post a Comment