Henry Joseph Shindika enzi hizo akiwa nahodha wa Taifa stars
Na Baraka Mpenja, Dar es
salaam
MANAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars,
Henry Shindika na Meck Mexime wamewataka wachezaji wa Stars kujituma katika
mchezo wa jumapili dhidi ya Zimbabwe.
Joseph amesema kuwa cha msingi kwa wachezaji wa Stars ni kwenda
kufanya kazi kama walivyofundishwa na kocha wao.
“Kocha ni mpya na ni mechi yake ya kwanza ya mashindano. Wachezaji
wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma zaidi”.
“Watanzania nao waipe sapoti timu yetu. Bado tuna safari ndefu,
hivyo ni lazima kuwaunga mkono vijana wetu”. Alisema Joseph.
Joseph aliongeza kuwa Zimbabwe ni timu nzuri kwasasa na
kitakachotakiwa kwa wachezaji wa Stars ni kuwa na nidhamu ya mchezo.
“Wachezaji watatakiwa kulinda lango,kucheza mpira na kushambulia
kwa nguvu zaidi kwasababu matokeo mazuri ya nyumbani yatawapa nafasi nzuri ya
kusonga mbele”. Alisema Joseph.
Naye Mexime kwa apande wake amesema ni kwa muda mrefu Taifa stars
haijapata matokeo mazuri, hivyo wachezaji watambue kuwa watanzania
wanawategemea sana kupata ushindi.
Mexime alisema kwasasa kinachotakiwa ni uvumilivu kwasababu kocha
ni mpya na kuna mambo yatabadilika.
“Kama wachezaji watajitambua na kucheza kwa kutumia nafasi
watakazopata badi watashinda”.
“Watanzania lazima tukubali kuisapoti timu yetu siku ya jumapili”.
Meck Mexime |
Wakati huo huo, kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema wachezaji
wake wako tayari kwa ajili ya mechi ya Kombe la Afrika dhidi ya Zimbabwe
(Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nooij amesema ujio wa washambuliaji Mbwana Samata na Thomas
Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
(RDC) kutaongeza morali ya kikosi chake.
Samata na Ulimwengu watawasili nchini Jumamosi mchana, saa 7.30
mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines wakitokea Khartoum, Sudan ambapo leo
(Mei 16 mwaka huu) wanacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Hilal ya
huko.
Wachezaji waliopo kambini kwa sasa ni Deogratias Munishi, Aishi
Manula, Said Moradi, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Nadir Haroub,
Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Himid Mao, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri
Kiemba, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Khamis Mcha,
Ramadhan Singano, John Bocco, Elias maguli na Kelvin Friday.
Wakati huo huo, timu ya Zimbabwe (Mighty Warriors) inawasili kesho
alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa
watu 27. Kesho saa 4 asubuhi (Mei 17 mwaka huu) Kocha wa timu hiyo atakuwa na
mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF).
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zinaanza kuuzwa kesho (Mei 17 mwaka
huu) kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers
uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, OilCom Ubungo, Uwanja wa Taifa, kituo cha mafuta
Buguruni na Dar Live Mbagala. Viingilio ni sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000
tu.
0 comments:
Post a Comment