Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya
Irani na Qatar, Helena Costa ametengeneza historia mpya kwenye soka nchini
barani ulaya.
Klabu ya ligi daraja la kwanza ya Ufaransa
Clermont imeweka historia mpya kwenye soka la nchi hiyo kwa kumtangaza
mwanamama Helena Costa kuwa kocha wao mpya kuanzia msimu ujao, na kumfanya kuwa
mwanamke wa kwanza kufundisha soka la hadhi ya juu nchini Ufaransa.
Costa, 36, alikuwa kocha wa timu ya taifa ya
wanawake ya Irani tangu mwaka 2012 lakini sasa amekubali kumrithi Regis Brouard
kwenye klabu ya Clermont.
Helena ambaye ni raia wa Ureno, aliwahi kufanya
kazi kama kocha mkuu wa kituo cha soka cha klabu ya Benfica na timu kadhaa
nyingine nchini Ureno, ambapo aliweza kushinda makombe kadhaa. Pia aliwahi
kuifundisha timu ya wanawake ya taifa ya Qatar.
0 comments:
Post a Comment