AFP Sports ameweka maswali 10 ambayo yatajibiwa siku ya mwisho:
1. Manchester City wanaweza kutwaa ubingwa?
Baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa siku ya jumatano, Manchester City wanahitaji pointi moja tu katika mchezo wa nyumbani dhidi ya West Ham ili kutwaa taji msmu huu.
Kama City watatoka sare, Liverpool watahitaji kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Newcastle angalau kuanzia mabao 13 kwa bila ili kutwaa ubingwa.
Lakini kama City watapoteza. Liverpool watafuta ukame wa kutobeba kombe kwa miaka 24 kama watashinda mechi yao.
2. Man City au Liverpool watavunja rekodi ya kufunga magoli?
Ushindi wa City wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa uliwafanya wafikishae magoli 100, huku nayo sare ya 3-3 waliyopata Liverpool dhidi ya Crystal Palace ikiwafanya wafikishe mabao 99.
Timu zote zipo katika nafasi ya kuvunja rekodi ya Chelsea ya mabao 103 waliyopata wakiwa chini ya Carlo Ancelotti msimu wa 2009-10.
Kama Liverpool watafunga goli moja, itakuwa mara ya kwanza kwa timu mbili kumaliza ligi kwa mabao 100 tangu 1960-61 ambapo Tottenham Hotspur, Wolverhampton Wanderers, Burnley walifanya hivyo.
3. Je, Luis Suarez anaweza kuandika rekodi mpya?
Akiwa na magoli 31 msimu huu, mshambuliaji huyu wa Liverpool ameshafikia rekodi za watu katika mechi 38 za ligi kuu alizocheza mpaka sasa na kuungana na Alan Shearer na Cristiano Ronaldo.
Kama atapiga Hat-trick ataifikia rekodi ya mabao 34 waliyofunga Shearer na Andy Cole katika mechi 42 za ligi kuu.
4. Je, Tottenham atawapisha Manchester United kucheza ligi ya Europa?
Tottenham wanahitaji ushindi katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Aston Villa ili kupata nafasi ya kucheza ligi ya Europa. Kama watapoteza, halafu Man United wakashinda dhidi ya Southampton, United watapanda juu yao kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
5. Je, Ryan Giggs anaweza kumaliza kibarua chake kwa ushindi?
Baada ya msimu mbaya na kupoteza ubingwa, huku wakishindwa kufuzu UEFA kwa mara ya kwanza tangu 1995, United watahitaji kumaliza kampeni zao msimu huu kwa ushindi dhidi ya Southampton.
Wakati Louis van Gaal akitarajiwa kutangazwa siku chache zijazo kuwa mrithi wa David Moyes, itakuwa nafasi ya mwisho kwa kocha wa muda, mkongwe Ryan Giggs.
6. Je, kuna mchezaji yeyote atakosa kombe la dunia?
Mlinzi wa Manchester United, Phil Jones ndiye mchezaji aliyeumia siku za karibuni baada ya kupata majeruhi ya bega katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Hull City siku ya jumanne.
Wachezaji wenzeka, Phil Jagielka (Everton) na Jack Wilshere (Arsenal) ni miongoni mwa wachezaji wasiokuwa na matarajio ya kucheza mechi za kombe la dunia.
7. Norwich City wanaweza kupona kushuka daraja?
Ushindi wa mabao 2-0 walioupata Sunderland katika uwanja wao wa nyumbani katikati ya wiki unamaanisha kuwa Nowrich City kimahesabu wameshashuka daraja.
Timu hii ipo nafasi ya nne toka mkiani, huku wastani wa mabao ukiwa -32 kwa -15 na West Brom. Mechi ya mwisho dhidi ya Asernal katika uwanja wa nyumbani itaamua hatima ya Nowrich.
8. Stoke City na Crystal Palace watamaliza katika nafasi zipi?
Stoke City wanaweza kumaliza katika nafasi 10 za juu tangu walipofanya hivyo msimu wa 1974-75 ambapo walimaliza nafasi ya tano.
Kwa mahesabu, wanaweza kumaliza nafasi ya 10 au 9 kama wataweza kuwafunga West Brom, halafu kikosi cha Alan Pardew kikimpiga iverpool.
Crystal Palace waliopo nafasi ya 11 tayari wameshaweka rekodi ya kumaliza nafasi ya juu zaidi tangu waliposhika kwa mara ya mwisho nafasi ya 10 mwaka 1991-92.
9. Nani ataaga ligi kuu?
Nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic atacheza mechi yake ya mwisho kabla ya kuondoka Old Trafford , wakati wachezaji wenzake Giggs, Patrice Evra na Rio Ferdinand siku chache zijazo watamaliza mikataba yao.
Wakongwe wa Chelsea, John Terry, Frank Lampard na Ashley Cole wanatarajia kucheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Cardiff City.
Makocha wa Tottenham, Tim Sherwood na Aston Villa, Paul Lambert wanaweza kuziongoza timu zao kwa mara ya mwisho.
10. Cardiff City watashuka daraja kwa ushindi?
Cardiff wanaburuza mkia na wataenda kucheza mechi ya mwisho wakiwa wameshashuka daraja, lakini wataingia kwa lengo la kuwamaliza wachovu wenzao Fullham katika mchezo wa nyumbani.
0 comments:
Post a Comment