


Wayne Rooney ana uhakika wa kuitwa
KOCHA
wa timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson amesema wachezaji wa Manchester United
wapo hatarini kutojumuishwa katika kikosi chake kinachotarajia kwenda Brazil kushiriki
kombe la dunia kuanzia juni 12 hadi juli 13 mwaka huu.
Bosi
huyo wa Simba watatu ameonya kuwa wachezaji Michael Carrick, Danny Welbeck,
Phil Jones, Chris Smalling, Ashley Young na Tom Cleverley wanaweza kutupwa nje
ya kikosi chake kwasababu ya kiwango kibovu cha klabu yao msimu huu.
Welbeck
na Carrick – kwa pamoja walifanya kazi nzuri wakati wa kampeni za kufuzu
fainali za kombe la dunia, lakini kiwango kibovu cha klabu yao kitaathiri
nafasi yao.
Hodgson
amesema atachukua wachezaji wa kikosi chake kwa kuangalia kiwango cha klabu
zao, hivyo amesema timu kama Manchester United wachezaji wake wanaweza kukosa
nafasi.
“Manchester
United ni moja ya klabu chache zenye wachezaji wengi timu ya taifa, lakini
wachezaji lazima wakubali bahati mbaya katika soka lao la England”. Amewaambia The Independence.
“Kama
klabu yao inafanya vibaya maana yake na wao hawafanyi vizuri. Kuna wachezaji
wengi wanaofanya vizuri katika klabu zao, kwahiyo inawatishia nafasi yao katika
kikosi cha timu ya taifa”.
“Nina uhakika wachezaji wa Manchester United
watanielewa kuwa hawana nafasi nzuri ya kucheza timu ya taifa kwa sasa,
kwasababu kiwango chao sio kizuri”.
“Ni
wajibu wangu kuchagua wachezaji wenye viwango bora kwa kazi tuliyonayo mbele
yetu”
Wayne
Rooney hayuko fiti sana, kwahiyo nafasi
yake ya kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Italia ipo kutegemeana na
atakavyoimarika.
Carrick,
Welbeck, Jones and Smalling bado wana
uhakika kidogo kuitwa, lakini Cleverley na Young wapo katika hatari ya kukosa kabisa.
Hodgson
atataja kikosi chake mei 12 mwaka huu baada ya kumalizika kwa ligi kuu soka
nchini England.
0 comments:
Post a Comment