Wakati
umefika: Neymar akiangalia kwa hisia kali wakati kikosi cha timu ya
taifa ya Brazil kikitaja `laivu` tayari kwa fainali za kombe la dunia
mwaka huu.
JE, umewahi kujiuliza itakuwaje siku ukisikia umechaguliwa kucheza fainali za kombe la dunia?
Wakati
huo haitakuwa kitu kingine bali ni ndoto ya kuonwa na mashabiki wengi
wa soka duniani kote, lakini kwa nyota wa FC Barcelona, Neymar na Dani
Alves ndoto zao zimekuwa kweli siku ya jumatano wiki hii.
Wachezaji
hao walipigiwa simu na kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Luis Felipe
Scolari kuwa wameteuliwa katika kikosi cha timu ya taifa kitakachokuwa
mwenyeji wa kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu.
Nyota hao walifurahi kupita maelezo na walinaswa na kamera ya Jo Amancio anayejulikana kuwa ni kaka yake Neymar.
Bosi wa Brazil Luis Felip Scolari akiwa katika mkutano na waandishi wa habari Laivu kwenye TV wakati wa kutaja kikosi chake
Wamepumua: Neymar baada ya kuona yupo kwenye kikosi cha Scolar alilipuka na tabasamu kubwa
Kuna mtu alikuwa anamwambia anaenda kombe la dunia! Dani Alves alijibu kwa utulivu habari hiyo
Nyota
hao wa Samba walirekodiwa wakimwangalia `laivu` Scolari anapotaja kikosi
cha timu ya Taifa ya Brazil na Neymar alionekana kuwa na furaha kubwa
baada ya kutajwa katika fainali hizo za kihistoria kwake.
Mshambuliaji
huyo wa Barcelona amelibeba taifa lake begani na ndiye mchezaji
anayetegemewa zaidi safu ya ushambuliaji ya Brazil mwaka huu.
Japokuwa Alves alikuwa mtulivu katika Camera, lakini bado furaha yake imebaki moyoni mwake na itaonekana Maracana mwezi juni na julai.
0 comments:
Post a Comment