
Majanga: Kocha wa Chelsea Jose Mourinho aliwaka mno kutokana na uzembe wa wachezaji wake hasa dakika 45 za kipindi cha kwanza za mechi ya ligi kuu soka nchini England iliyomalizika kwa suluhu pacha ya bila kufungana dhidi ya Nowrich City.
Matokoe hayo yameua matumaini ya Mreno huyo kutwaa ubingwa msimu huu na kuwaachia Man City na Liverpool wakichuana vikali.
Kama Mourinho anataka kushinda taji msimu huu anatakiwa kushinda mechi moja iliyosalia na kuwaombea Liverpool na Man City wapoteze mechi zote mbili walizasaliwa nazo.
Liverpool leo wanashuka dimbani kukabiliana na Crystal Palace.
Chelsea wapo nafasi ya tatu kwa pointi 79 baada ya kucheza mechi 37.

Hisia kali: Ashley Cole alishindwa kuzuia machozi pale mashabiki wa Chelsea waliposimama kutoa heshima kwake katika dimba la Stamford Bridge jana jumapili


Siku ya huzuni: Cole akimwaga machozi kwasababu kuna taarifa kuwa anaondoka Chelsea majira ya kiangazi mwaka huu kutokana na mkataba wake kumalizika na klabu haina mpango wa kumuongezea

Marafiki wazuri: Cole akikumbatiana na mchezaji mwenzake wa Chelsea Frank Lampard baada ya mechi ya jana dhidi ya Norwich
0 comments:
Post a Comment