Friday, May 2, 2014


Rui amepigwa marufuku ya mechi 6
Naibu wa kocha ya klabu ya Chelsea, Rui Farai amepigwa marufuku ya kutokutenda jukumu lake uwajani kama naibu wa kocha kwa jumla ya mechi sita na faini ya pauni £30,000 .
Mreno huyo alikirii makosa yake mawili ya kumkemea refa Mike Dean na kuzua vurumayi uwanjani na kupewa kadi nyekundu.
Kocha huyo alizua vurumai uwajani wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Sunderland tarehe 19 April.


Refa huyo aliwapa Sunderland penalti ambayo iliwafanya klabu ya Sunderland kushinda mechi hiyo kwa mabao mawili kwa moja (2- 1).
Marufuku hiyo ilijumlisha mechi mbili za nyumbani zilozobakia msimu huu dhidi klabu ya Norwich na Cardiff na nne katika msimu mpya .
Naye kocha mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho pia anakabiliana na makosa ya utovu wa nidhamu kwa kutumia kinaya kumkejeli na kumpongeza refa Mike Dean na msaidizi wake Mike Riley.
Haya yanajiri baada ya kiungo cha kati Ramires kupigwa marufuku kutoshiriki mechi nne kutokana na kitendo cha kumgonga kumbo mchezaji wa Sunderland Larsson wakati wa mechi hiyo.
Chanzo: Bbcswahili

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video