KOCHA wa muda wa Manchester United, Ryag Giggs
amethibitisha kuwa Wayne Rooney na Phil Jones watakuwa fiti kuitumikia England fainali
za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Jones aliumia katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Hull
City Old Trafford jumanne ya wiki hii, wakati Rooney amekosa mechi mbili zilizopita
za ligi kuu soka nchini England na yuko
hatarini kukosa mechi ya mwisho dhidi ya Southampton.
“Majeruhi ya Phil sio kubwa sana . Hatakuwepo
mechi ya jumapili, lakini atakuwa sawa kwa fainali za kombe la dunia.” Alisema Giggs
mwenye miaka 40.
Giggs alieleza kuwa Rooney amefanya mazoezi wiki
hii, lakini alikiri kuwa yupo mashakani kucheza dhidi ya vijana wa Mauricio
Pochettino.
Kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya taifa ya taifa
ya England kitakachoshiriki kombe la dunia kitatajwa jumatatu na kocha mkuu Roy
Hodgson kabla kwenda Ureno kuweka kambi.
England watarejea Wembley mei 30 kujipima ubavu na
Peru kabla ya kucheza dhidi ya Ecuador na Honduras.
Vijana wa Hodgson wapo kundi D na wataanza mechi ya ufunguzi juni 14 mwaka huu dhidi ya Italia.
Vijana wa Hodgson wapo kundi D na wataanza mechi ya ufunguzi juni 14 mwaka huu dhidi ya Italia.
0 comments:
Post a Comment