RYAN Giggs anaweza kupata kazi ya kudumu Manchester United baada ya kocha anayetarajia kujiunga na Mashetani wekundu, Louis Van Gaal kuweka wazi kuwa huwa anapenda kumuacha kocha mmoja aliyekuwa katika kikosi chake kipya kabla ya kujiunga na kuanza kazi rasmi.
Giggs alishuhudia timu yake ikimaliza mechi ya mwisho kwa sare ya 1-1 na Southampton jana.
Sasa kinachosubiriwa ni kuona nini Van Gaal ataamua kuhusu hatima ya Giggs mara atakapothibitishwa kuwa kocha wa United baadaye wiki hii.
Lakini kutokana na falsafa ya Mholanzi huyo kubakisha moja ya makocha waliokuwepo imetoa matumaini kwa Giggs kupata ajira ya kudumu.

Kazi kubwa: Louis van Gaal ana kazi kubwa kombe la dunia kabla ya kujiunga na Manchester United.
Alipoulizwa nani alikuwepo nyuma ya mandeleo ya Thomas Muller katika klabu ya Bayern Munich, Van Gaal alisema: "Ninapojiunga na klabu mpya, mara zote huwa nambakisha kocha mmoja kutoka benchi lilikokuwepo".
"Nikiwa Bayern nilimbakisha Herman Kerland ambaye mpaka sasa anafanya kazi chini ya Pep Guardiola".
"Napenda kujua nani ametokea katika mfumo wa soka la vijana. Siku zote nahitaji kujua hilo".
"Herman ndiye aliyeniambia: "Muller, Badstuber na Alaba. Hawa ni wachezaji wazuri".
"Namuachia afanye mazoezi na kikosi cha kwanza, nachunguza-halafu naamua watacheza wapi".
Kwasasa Van Gaal ni kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi na sasa anaiandaa timu yake kwa ajili ya mechi ya kirafiki wikiendi hii dhidi ya Ecuador
Giggs akiwa benchi kwenye mechi dhidi ya Southampton, wengine ni wasaidizi wake Nicky Butt, Paul Scholes na Phil Neville

Tabasamu kubwa: Ryan Giggs anaweza kubakishwa kwenye benchi la ufundi msimu ujao
0 comments:
Post a Comment