RYAN
Giggs anatarajia kumwambia kocha anayekuja kujiunga na Manchester United, Louis Van Gaal kuwa anahitaji kuendelea
kucheza na kumalizia soka lake Old Trafford kwa msimu mwingine.
Giggs
aliyepewa mikoba ya ukocha mkuu Man United baada ya David Moyes kutimuliwa
mwezi uliopita, alicheza dakika 20 za mwisho katika ushindi wa 3-1 dhidi ya
Hull City jumanne usiku, huku wengi wakiamini kuwa mechi hiyo ilikuwa ya mwisho
kwake kucheza Old Trafford.
Lakini
mkongwe huyo mwenye miaka 40 bado anajiona kuwa na nguvu za kuendelea kushiriki
mikikimikiki ya ligi kuu nchini England
na taarifa kutoka Carrington zinasema kuwa hakuna sababu ya Giggs kutoendelea
kucheza na kuifundisha klabu hiyo kwa msimu ujao.
Van
Gaal anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa United wiki ijayo na hatima ya
baadaye ya Giggs haijulikani kwani mpaka sasa Mholanzi huyo hajataja majina ya
watakaokuwa wasaidizi wake.
United
wamepokea vizuri mwanzo wa Giggs klabuni hapo, lakini maamuzi ya mwisho juu ya
kocha huyo mchezaji kuendelea kuwepo benchi la ufundi msimu ujao yapo juu ya
Van Gaal.
Kocha
msaidizi wa timu ya taifa ya Uholanzi, Patrick Kluivert hatajumuika na Van Gaal
Old Trafford na hii inatoa nafasi kubwa kwa Giggs kupewa ofa ya kuwa kocha
msaidizi.
Tangu
apewe ukocha mkuu wa muda kurithi mikoba ya Moyes, Giggs ameiongoza Man United
kushinda mechi mbili Old Trafford dhidi ya Nowrich City na Hull City, lakin
aliachwa mdomo wazi baada ya kufungwa bao 1-0 na Sunderland.
0 comments:
Post a Comment