
Wakizitawanya: Mayweather akihesabu dakika, huku warembo wakishindana kuhesabu haraka dola laki moja kitandani kwa bondia huyo.
BONDIA
Floyd Mayweather ameonesha jeuri ya pesa ndefu baada ya kuchukua
warembo wawili na kuwashindanisha kuhesabu pesa zinazofikia dola laki
moja akiwa kitandani kwake, huku akitumia saa yake kuangalia nani
anahesabu haraka zaidi.
Mayweather
alishinda mchezo jumamosi iliyopita dhidi ya Marcos Maidana mjini Las
Vegas na kuchukua ubingwa uzito wa welterweight na kuendeleza rekodi ya
kutofungwa katika michezo 46 ya kimataifa na ameshangilia ubingwa wake
kwa kuwashindanisha warembo kuhesabu `mkwanja` wake.
Mmarekani huyo akiwa na kibegi kidogo chenye saa 18 aliandika maneno yafuatayo: ” @thatjessilee
na @badmedina wanacheza mchezo, kuona nani anaweza kuhesabu dola laki
moja ( $100,0000) kwa haraka zaidi. Hivi ndivyo wanafanya wakichoka.
#TheMoneyTeam #FollowBeautifulLadies’.
Ni
haki yake kusema dola laki moja ni fedha kidogo kwa bondia huyo bingwa
mara tano wa dunia, ambaye alipata dola milioni 70 kutokana na pambano
lake dhidi ya Maidana.
Alipata
dola milioni 32 kenye mchezo uliopigwa MGM Grand , na vilevile anasema
anapata dola milioni 38 kutokana na matangazo ya televisheni.
Wanawake wawili, Jessi Lee na Doralie Medina walipigwa picha wakiwa kama sehemu ya wasaidizi wa timu ya Mayweather, inayojulikana kama Timu ya hela ` The Money Team (TMT)`.

Timu
ya hela: Doralie Medina, anayejulikana kwa jina la ‘badmedina’ ni
mmoja wa wasichana waliokuwa wanashindana kuhesabu mkwanja wa
Mayweather

Mwaliko wa sherehe ya kuzaliwa ya Medina iliyoandaliwa na Timu ya hela mjini Las Vegas
Medina, akionekana amepumzika. Hii picha ipo katika akaunti yake ya Instagram
Msichana mwingine aliyeshindana kuhesabu pesa za Mayweather ni Jessi Lee

Mapambo: Nyota wa masumbwi, Floyd Mayweather alionesha picha yake ya vito vyake Instagram mwezi uliopita
0 comments:
Post a Comment