TAARIFA za uhakika zilizoufikia mtandao huu dakika
chache zilizopita ni kwamba kocha mkuu wa Young Africans, Mholanzi, Hans Van
der Pluijm amepata kazi mpya nchini Saudi Arabia.
Pluijm aliyejiunga na Yanga mapema januari mwaka
huu umepata shavu hilo katika klabu ya Al Shoalah FC inayoshiriki ligi kuu soka
nchini humo.
Kocha huyo anaondoka baada ya kushindwa kutetea
ubingwa na kuzidiwa kete na kocha wa Azam fc Joseph Marius Omog msimu huu ambao
Yanga walimaliza katika nafasi ya pili.
Pluijm alirithi mikoba ya mholanzi mwenzake, Ernie
Brandts aliyetimuliwa mwezi desemba mwaka jana baada ya kufungwa mabao 3-1 na
Simba sc katika mechi ya Nani Mtani Jembe.
Hata hivyo, Pluijm alikuwa na mtababa mfupi wa
miezi sita na Yanga ambao unatarajia kumalizika mwezi ujao.
Sasa Yanga wanaingia katika kibarua kingine cha
kusaka kocha mkuu atakayesaidiana na kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.
Mtandao huu unaendelea kufuatilia taarifa hii na
baadaye utapewa habari nzima. Tafadhali endelea kuwa nasi.
0 comments:
Post a Comment