BEKI wa kushoto wa Manchester United, Mfaransa
Patrice Evra amesema itawauma sana pale nahodha wao, Nemanja Vidic atakapoondoka
klabuni hapo na kujiunga na Inter Milan majira ya kiangazi mwaka huu.
Uhamisho wa Vidic kwenda Italia ulithibitishwa
mwezi machi mwaka huu baada ya nyota huyo kugoma kuongeza mkataba Man United.
Mserbia huyo akiwa na United ameshsinda makombe
matano ya ligi kuu na UEFA mwaka 2008.
Evra ambaye anaweza kujiunga na mserbia huyo
katika klabu ya Inter majira ya kiangazi, amecheza kwa muda mrefu na Vidic
tangu wote kwa pamoja wajiunge na Manchester United wakati wa dirisha dogo la
usajili mwaka 2006.
Mfaransa huyo naye anamaliza mkataba wake majira
ya kiangazi mwaka huu na bado anapima hatima ya namba yake msimu ujao ili kuamua
kubaki au kuondoka.
“Inauma sana kumpoteza Vida.” Mfaransa huyo
ameiambia tovuti ya United. “Kwa mimi, ni beki bora zaidi wa kati. Unapoona mchezaji
kama Vidic anaondoka klabuni, inahuzunisha sana”.
“Unapozungumzia Vida, kama unanizungumzia mimi.
Tulijiunga na klabu pamoja. Nakumbuka mechi ya kwanza ilikuwa ngumu sana. Katika
mechi moja wote tulikuwa wachezaji wa akiba. Tulikuwa na kiwango cha chini.
“Rene Meulensteen alikuwa kocha wa wachezaji wa
akiba na alituchukua wote. Tulikuwa tunazungumza kwenye vyumba vya kuvalia
nguo: “ Oh mwanangu, kwanini tumekuja Manchester?, tungebaki katika klabu zetu
za zamani”.
“Ilikuwa wakati mgumu sana, lakini tuliimarika kwa
pamoja. Tulikuwa tunalala hoteli moja na kwenda mazoezini pamoja, tulishinda
mataji pamoja. Kiukweli nahuzunika sana kumpoteza”. Alisema Evra.
0 comments:
Post a Comment