MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Edin Dzeko
amesema klabu yake itajituma na kucheza kwa `asilimia 200` katika mechi mbili
zilizosalia.
Sare ya 3-3 waliyoipata Liverpool jumatatu ya wiki
hii, imewafanya City wawe na asilimia
kubwa ya kuchukua ubingwa kama watashinda mechi ya leo usiku dhidi ya Aston
Villa katika uwanja wa Etihad.
Endapo City watazoa pointi tatu watakuwa mbele kwa
pointi mbili dhidi ya majogoo wa jiji wenye pointi 81.
Dzeko aliyefunga bao muhimu mwaka 2012 dhidi ya
QPR na kuchangia kuipa ubingwa Man City
amesisitiza kuwa wamejifunza kutokana na
matokeo ya mechi za mwishoni.
“Tutajitahidi kufanya kila linalowezekana na
tunadhani tayari tumeshafanya kazi kubwa,” mshambuliaji huyo amekaririwa na
gazeti la The Sun.
“Baada ya kushinda Goodison jumamosi ( 3-2 dhidi
ya Everton), tunaenda kucheza mechi mbili za mwisho nyumbani dhidi ya Villa na
West Hall, si kwa asilimia 100, ni asilimia 200 tutajitahidi kushinda”.
“Kila kitu kipo mikononi mwetu kama miaka miwili
iliyopita. Nakumbuka tuliposhinda ubingwa dhidi ya QPR, kila mtu alitegemea
tungeshinda kirahisi. Ilikuwa ngumu mpaka dakika ya mwisho”.
“Nadhani tumejifunza kitu fulani. Tunajua si
vizuri kuidharau timu na tunatakiwa kufanya kazi yetu vizuro”.
Dzeko ameifungia Man city mabao 14 katika mechi 29
za ligi kuu alizocheza msimu huu.
0 comments:
Post a Comment