Anarudi: Lukaku amefunga mabao 15 katika mechi 32 alizoichezea Everton msimu huu.
Japokuwa alifunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Liverpool na bao la ushindi dhidi ya PSG katika michuano ya UEFA, Ba bado hana nafasi ya kubakia Chelsea.
Wazee wa darajani wanatarajia kuleta angalau mshambuliaji mmoja majira ya kiangazi mwaka huu.
Vijana wa Merseysiders walituma maombi ya kumsajili nyota huyo wa Senegal msimu uliopita kabla ya kupewa Lukaku kwa mkopo lakini sasa wana mpango wa kutuma ofa nyingine tena kwa Ba.
Everton wanahitaji kuongeza nguvu katika kikosi chao kwa ajili ya michuano ya ligi kuu na Europa msimu ujao.
Chelsea imeripotiwa kuwa tayari imeshamwabia Demba Ba kuwa ataondoka klabuni hapo, wakati huo huo mshambuliaji huyo amethibitisha kuondoka baada ya kushindwa kupata mafanikio chini ya Jose Mourinho.
West Ham, Arsenal, West Brom na Fenerbahce pia zinahusishwa kutaka kuinasa saini ya nyota huyo.
0 comments:
Post a Comment