Saturday, May 3, 2014



 BRENDAN Rodgers bado anasubiria mshambuliaji wake Daniel Sturridge awe fiti tayari kwa safari ya kuwafuata Crystal Palace katika mchezo muhimu wa ligi kuu nchini England siku ya jumatatu wiki ijayo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England alitolewa nje katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester city, aprili 13 mwaka huu kutokana na majeruhi ya nyama za paja na wiki iliyofuata  alikosa mechi dhidi ya Nowrich ambayo Liverpool walishinda mabao 3-2.

Sturridge alianzia benchi na kuungizwa baadaye katika mechi ya jumamosi iliyopita dhidi ya Chelsea na kushuhudia klabu yake ikilala mabao 2-0 na kuwa hatarini kukosa ubingwa ambao hawajabeba kwa miaka 24 sasa.

Katika mkutano wa jana jioni na waandishi wa habari, Rodgers alikiri kuwa mechi na Chelsea nyota wake hakutakiwa kucheza na kuelekea mchezo muhimu wa jumatatu kwenye uwanja wa Selhurst Park wanasubiria kuimarika kwake.

“Tutaangalia ndani ya saa 48 zijazo. Hajafanya mazoezi tangu alipopata majeruhi, kidogo ilikuwa kazi ngumu kwake dhidi ya Chelsea”. Rodgers aliwaambia waandishi wa habari.

“Tulifanya jitihada kubwa ili kumrudisha na tulihitaji awepo hata benchi, lakini kwa bahati mbaya haikutusaidia”.

“Anapokuwa katika hali nzuri anafanya kazi kubwa. Amekuwa karibu zaidi na madaktari wa klabu wiki hii. Ataungana na wenzake, lakini tutaona jinsi itakavyokuwa jumatatu”. Aliongeza Rodgers.
 http://gool.net/wp-content/uploads/2014/04/Player-of-the-year-Luis-Suarez.jpg
Mshambuliaji mwenzake na Sturridge, Luis Suarez alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa PFA nchini England jumapili iliyopita baada ya kufunga mabao 30 katika mechi 31 za ligi kuu.

Rodgers alikiri kuwa mshambuliaji wake huyo raia wa Uruguay alipambana sana na kustahili tuzo hiyo kwasababu kwa wakati wote amekuwa katika kiwango cha juu.

“Hongera zake. Ilikuwa zawadi iliyotokana na jasho lake”, Aliongeza kocha huyo wa zamani wa Swansea City.

“Amekuwa na kiwango kikubwa katika klabu msimu huu”.

“Kwahiyo alistahili na najua ana heshimu sana tuzo hiyo, kutokea miongoni mwa wachezaji wengi wa nchi hii si kazi nyepesi. Najua ana furaha”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video