Monday, May 19, 2014



10357474_634079413340945_8148690486284095511_n
Na Baraka Mbolembole
Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua inayofuata kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, nchini, Morocco. Stars iliichapa,timu ya Taifa ya Zimbabwe ' The Warrios' kwa goli 1-0, siku ya jana katika mchezo wa kwanza wa mashindano kwa kocha mpya wa kikosi hicho, Muholanzi, Martin Nooij.
Goli la dakika ya 13 lililofungwa na mshambulizi wa kati, John Bocco lilifanya kikosi hicho kinachowania kufuzu kwa mara ya kwanza fainali za Afrika tangu mwaka 1980 kuhitaji sare ya aina yoyote ili kusogea katika hatua ya makundi. Mara ya mwisho, Stars ilifuzu kwa fainali za Afrika miaka 34 iliyopita nchini, Nigeria ikiwa na kikosi kilichoongozwa na rais aliyepita wa Shirikisho la soka nchini, TFF, Ndugu, LeodgarTenga, Mtemi Ramadhani, meneja wa muda mrefu wa timu hiyo , Leopard Tasso Mukebezi na nyota wengi wa soka la Tanzania wakati huo.
Katika mchezo wa jana, kocha, Nooij aliwaanzisha washambuliaji watatu, Bocco, ambaye alikuwa akizungukwa naThomas Ulimwengu aliyekuwa akishambulia akitokea upande wa kulia, na Mbwana Samatta. Na wote watatu walihusika kwa goli pekee lililopatikana ambalo litaipeleka timu, National Sports Stadium, Harare ikiwa inajiamini.Samatta alitoa pasi ya kichwa kwa Ulimwengu ambaye alipiga pasi safi ya mwisho kwa mfungaji, Bocco ambaye aliachia ' kiki kali' ya karibu. Ilikuwa ni goli ' bab-kubwa' ambalo lilipangwa na wachezaji wenyewe.
Kwa muda mrefu, Stars imekuwa ikiangushwa na wachezaji wa kikosi cha kwanza kushindwa kudumu katika viwango vyao wanapokuwa klabuni na kufanya timu hiyo kuwa na mabadiliko kila wakati.Ila,namtazama kocha, Nooij na kumuona mwenye bahati kubwa kuwa na wachezaji ambao walifanya kazi na makocha waliopita, Marcio Maximo, Jan Poulsenna Kim Poulsen. Samatta na Ulimwengu wamekuwa wakicheza nje ya Tanzania kwa miaka mitatu tena katika klabu bora barani Afrika, japo walikuwa na uchovu wa kuiwakilisha, TP Mazembe katika michuano ya ligi ya mabingwa, siku ya ijumaa iliyopita, wawili hao wanaweza kumsaidia, Nooij katika mipango yake.
Itapendeza kama, Bocco ataendelea kuwa katika kiwango chake cha sasa kwa muda mrefu ujao, kwani itaifanya timu hiyo kuwa na uhakika wa kufunga magoli, mshambulizi huyo wa klabu ya Azam FC,anashabaha akiwa klabuni kwake lakini alikuwa akishindwa kujiamini anapokuwa Stars. Kwa miaka minne sasa yupo, Stars hivyo anatakiwa kujiamini na kuhimili presha ya mashabiki kila anapokuwa akipoteza nafasi.

MartNooijKocha mkuu wa Taifa stars, Mart Nooij

Kwa namna mchezo wa jana ulivyokuwa, Stars iliundwa na wachezaji 10 kati ya 11 walioanza mchezo ambao tayari wamekuwa katika timu hiyo kwa miaka mitatu na kuendelea, kiungo Frank Domayo ana miaka miwili katika kikosi hicho na tangu alipoingia kwa mara ya kwanza, mwaka 2012 amekuwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza. Hakuwa katika kiwango chake cha kawaida katika mchezo jana, alipoteza mipira mingi,hakuwa akiisogeza timu mbele, na pasi zake nyingi hazikufika.Ila, bado ni mchezaji anayebeba matumaini ya muda mrefu katika safu ya kiungoya Stars kwani ndio kwanza anakaribia miaka 21. Akishirikiana na Mwinyi Kazimoto, pamoja na Mrisho Ngassa, safu ya kiungo ya Stars ilionekana kupotea wakati Fulani uwanjani na kuwafanya, viungo wa Zimbabwe, Rendai Ndoro, Milton Nauba,Kudakwashe Mahadina Cuthbert Malajila kutengeneza zaidi nafasi tatu katika uwanja wa ugenini.
Ushindi wa goli moja ni ' kiduchu ' lakini unatosha kupunguza presha. Kufunga goli moja ugenini itakuwa ni sawa na kuwapa mlima mrefu zaidi wapinzani kuupanda.Ila, wakati kocha wa ' The Warrios', Ian Gorowa akisema timu yake ilikosa bahati ya kushinda japo walifanikiwa kutengeneza nafasi za kutosha, Yule wa Stars, Nooij yeye kwa upande wake amesema kuwa timu yake ilicheza vizuri na walishindwa kupata magoli ya kutosha kutokana na wachezaji kupoteza nafasi nyingi walizotengeneza.
Zimbabwe inahitaji ushindi wa magoli 2-0 na kuendelea ili wasonge mbele. Miaka miwili iliyopita, Stars ilitoka sare na Msumbiji katika mchezo wa nyumbani na wakalazimisha sare ugenini ila wakatolewa na kwa mikwaju ya penalty na kuondolewa katika harakati za kufuzu AFCON 2013.Wachezaji kadhaa bado wapo kikosini, akiwamo Samatta aliyekosa mkwaju wa penalti( wakati huo ) hivyo tayari wanao uzoefu wa michezo kama hiyo. Safu ya ulinzi ilicheza vizuri, japokuwa kuna matatizo katika baadhi ya maeneo. Nadir Haroub na patna wake, Kelvin Yondan waliweza kwenda sambamba na washambuliaji, Peter Moyona Eric Chipata.
Zimbamwe iliyokuwa bila wachezaji wake watatu wanaocheza katika klabu ya Kaizer Chiefs ya AfrikaKusini, washambuliaji, Knowledge Musona Knowledge  na Kingston Nkhatha , pamoja na kiungo mchezeshaji anayecheza pia katika klabu hiyo, Willard Katsande .Hivyo kocha wa Stars anatakiwa kutazama namna walinzi wake wapembeni walivyokuwa rahisi kupitika hasa kwa Shomari Kapombe aliyecheza kama mlinzi wa kulia. Oscar Joshua alikuwa akiichezea Stars mchezo wake wa kwanza wa mashindano, hakupanda sana na hilo lilisaidia safu nzima ya nyuma kutulia . Kama, Oscar angepotea zaidi kama ilivyokuwa kwa Kapombe katika kipindi cha kwanza, Stars ingekuwa na wakati mgumu zaidi. Ila utulivu umefanya timu kuwa na faida ya goli moja huku ikiwa haijaruhusu goli katika uwanja wa nyumbani.
Hii, siyo timu mpya, Ni timu ya muda mrefu ambayo kwa kiasi Fulani imekomaa kama wachezaji watafanya mambo yao kwa uhakika kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita. Nooij, aliamua kuwaanzisha wachezaji wanne kati ya watano wa klabu ya Yanga katika safu ya ulinzi na mpango huo ulitimia kwa kuwa, Kapombe aliweza kwenda sambamba na Oscar katika kipindi cha pili, huku Nahodha, Nadir na Yondan wakitimiza majukumu yao kama wachezaji wazoefu zaidi katika kikosi hicho ambao tayari wamefanya kazi na Maximo, Jan na KIM.
Stars imeweka mguu mmoja ndani, ila ni muhimu wachezaji kwenda ugenini kucheza zaidi ya walivyocheza katika mchezo wa kwanza. Goli moja itamaanisha kuwa wenyeji watahitaji kufunga magoli zaidi ya matatu ili wafuzu kwa hatua ijayo, ila tusisahau kuwa mechi inaweza kufika hadi hatua ya mikwaju ya penalty. Mechi ya kwanza ya Mwalimu, Martin Nooij, Stars imekuwa ni nzuri kimatokeo na kichezaji.
0714 08 43 08

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video