GWIJI wa
soka FC Barcelona, Johan Cruyff amesema Atletico Madrid wanastahili kushinda
taji la La Liga msimu huu.
Cruyff na Hristo Stoichkov walipewa nafasi ya
kutabiri timu gani itachukua ubingwa, lakini Crufy ameinyima nafasi timu yake
ya zamani ya Barcelona na Real Madrid.
Kwasasa Atletico wapo mbele kwa pointi tatu dhidi ya
Barca ambao watacheza nao mechi ya kufunga msimu.
Cruyff anaamini vijana wa Diego Simeone
watakaokutana na wapinzani wao wa mji katika fainali ya UEFA, wana nafasi ya
kuchukua `ndoo` na hata kama watakosa bado wanatakiwa kupongezwa kwa kuonesha
kiwango cha juu msimu huu.
“Atletico wanastahili kutwaa ubingwa na kama itatokea
wamekosa, watajipanga kwa msimu ujao”.
Aliwaambia waandishi wa habari.
Wakati huo huo itakuwa mbaya zaidi kwa Barcelona
kama watakosa ubingwa baada ya kutolewa na Atletico katika michuano ya UEFA
hatua ya nusu fainali.
Pia walipoteza mchezo wa fainali wa kombe la
mfalme ` Cope del Rey ` dhidi ya Real Madrid,na nyota huyo wa zamani wa Barca
alisema matokeo hayo ni udhaifu wa bodi isiyoelewa mpira.
“Maamuzi yanachukuliwa na watu wa juu na kufanya
yawe magumu kutekelezeka, kwasabau watu wa juu hawajui mpira”. Alisema.
“Siku zote kama unajua mpira, utagundua kwanini
mlifanya vizuri na sasa mnafanya vibaya”.
Nyota huyo wa zamani aliongeza: “sidhani kama Real
Madrid watashinda mataji yote matatu msimu huu”.
Kwa upande wake Stoichkov alitabiri kuwa wakatalunya
watabeba taji la Las Liga, huku Atletico Madrid wikiifunga Real Madrid kwenye
fainali ya UEFA.
“Inanikumbusha wakati Deportivo walipopoteza Riazor
(1992). Tulitegemea Deportivo hawashindi, na kwa mfano huu, Barca watakuwa mabingwa kama
watashinda mechi zao mbili”.
“Lolote linaweza kutokea, hii ni kweli; lakini
Barca watashinda La Liga na Atletico watashinda UEFA.”
“Madrid wana Copa del Rey. Hawana ubavu tena, na
walidhani wangeshinda makombe matatu, lakini hilo haliwezi kutokea”.
0 comments:
Post a Comment