
SERGIO
Busquets amekiri kuwa matumaini ya Barcelona kutetea ubingwa wao wa La Liga msimu
huu yamekwisha baada ya sare ya jana ya mabao 2-2 dhidi ya Getafe.
Barcelana
walianza kufunga mara mbili kupitia kwa Lionel Messi na Alexis Sanchez, lakini
Getafe walichomoa yote kupitia kwa Angel Lafita.
Bao
la dakika za lala salama la Lafita limewafanya Barcelona kuwa pointi tatu nyuma
ya vinara Atletico Madrid ambao wanaweza kufikisha pengo la pointi sita kama
watawafunga Levante leo jumapili.
“La
Liga kwetu tumeikosa. Kimahesabu hatuwezi”. Busquets amewaambia waandishi wa
habari.
“Kwa
wiki za karibuni hatujawa katika kiwango kizuri, lakini tulijitahidi kushinda
mechi zetu, matokea kama ya leo (jana) yanawezekana kutokea”.
“Tulimiliki
mpira na kupata nafasi za kufunga, tunatakiwa kujipanga zaidi na kucheza kitimu
ili kushinda mechi zijazo”.
Kocha
Tata Martino amekubali kubeba lawama zote kutokana na msimu mbaya kwa Barcelona,
lakini Busquets amesema wachezaji nao wanatakiwa kushirikiana na kocha kubeba
msalaba huu mzito kwao msimu huu ambapo wanaweza kumaliza bila kombe.
“Tulifungwa
mabao ambayo hatukustahili kufungwa. Makosa ni kwa timu nzima”. Alilaumu kiungo
huyo.
“Tumebakiwa
na mechi mbili na tutajitahidi kushinda kwasababu tunaichezea klabu bora zaidi
duniani”.
“Labda
msimu ujao tutakuwa wazuri zaidi”.
Barcelona
watasafiri kuwafuata Elche kabla ya kuwakaribisha Atletico Madrid katika
mchezo wa mwisho.
Kama
Atletico watashinda mechi zao mbili za mwisho, watakuwa wamefanikiwa kutwaa
ubingwa wa La Liga.
RATIBA YA LA LIGA LEO HII HAPA
SPAIN: Primera Division | |||||||
13:00 | Almeria | - | Betis | ||||
18:00 | Levante | - | Atl. Madrid | ||||
20:00 | Sevilla | - | Villarreal | ||||
22:00 | Real Madrid | - | Valencia |
0 comments:
Post a Comment